Mariam Mbewa Akiwa katika Moja ya Green House ambayo yeye Mwenyewe ameifanyia kazi hapa akifurahia Matunda yake...
Hapa akiendelea na mavuno ya nyanya.. Hii Green house waweza ona ilivyo katika Ubora wake.
Waswahili wanasema kwamba ukijibidisha zaidi utafanikiwa zaidi.. Na ukilala basi usitegemee pesa zitakufuata..
Pia wanasema kwamba Mwanamke anaweza hata Bila kuwezeshwa..
Tunapoendelea kutafakari haya hebu sote tutupie macho kwa Mjasiliamali ambaye yeye ameamua kujihusisha katika Kilimo Bora cha kisasa ambacho hakitumii nafasi kubwa na chenye mafanikio makubwa yaani Green house si Mwengine ni Mariam Mbewa ambaye kwa hakika amefanikiwa sana katika kifunga Green House katika mikoa mbali mbali ikiwemo Dodoma, Njombe na Dar es salaam kuitaja kwa uchache ingawa ipo mingi zaidi..
Mafanikio haya yamempelekea kujiamini na kuendelea kufikiria na Kuthubutu zaidi ambapo sasa Binti huyu ameanzisha mradi mpya na ambao ni wa ufugaji wa nyuki hii ni hatua kubwa sana, mafanikio yote haya ni kwa sababu tuu anajishughulisha na kuwa Mbunifu zaidi..
Huu ni mwanzo tuu lakini tutawaletea Taarifa zaidi za Mjasiliamali huyu .. Usikose
Imeandaliwa na Fredy Njeje Official Blog.
No comments:
Post a Comment