Lakini wakati hali ikiwa hivyo, bado wapo ambao wako kwenye uhusiano
lakini wamekuwa wakizitumia vibaya simu zao. Unakuta mume wa mtu lakini
ana namba za wanawake kibao kwenye simu yake na akiwa mbali na mwenza
wake, ni mwendo wa kuchati na kuongea nao mambo yao wanayoyajua.
Vivyo hivyo kwa wanawake, wapo ambao wana wapenzi lakini mawasiliano
na vijibwana vya nje yamekuwa yakiendelea kama kawaida.Hatari zaidi
inakuja pale ambapo unagundua kuwa hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza
kudiriki kumuachia mwenza wake simu yake kwa siku zima.
Achilia mbali kumuachia, hata kuigusa tu ugomvi mkubwa unaweza
kuibuka. Kwa nini? Kwa sababu ni watu wachache sana ambao simu zao
hazina madhambi.Sasa leo nataka niwape kisa kimoja ambacho naamini ni
fundisho kwa wenye tabia ya kuchati na michepuko wakati wakiwa mbali na
wapenzi wao.
Kijana mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sudi alikuwa na mke
wake. Alimpenda sana na kila wakati amekuwa akimwambia hivyo. Mbali na
kumwambia mkewe kuwa anampenda pia alimhakikishia kuwa, hata siku moja
hatadiriki kumsaliti.
Sudi alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja na mkewe alikuwa
mfanyabiashara. Kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda, Sudi akaanza
kubadilika, akawa ni mtu wa kubadili wasichana na mara nyingi amekuwa
akiwasiliana nao akiwa mbali na mkewe.
Siku moja ya Jumanne saa sita mchana wakati Sudi akiwa kazini alianguka ghafla. Akachukuliwa na kukimbizwa hospitalini na mkewe akapigiwa simu kupewa taarifa.
Mke akafika haraka na kumkuta mumewe hajitambui. Wakati jitihada za
kumtibu zikiendelea, mke akaomba apewe simu ya mumewe ili afanye
mawasiliano.Wakati mke akichukua ile simu, kumbe mume alishaanza
kuwasiliana na michepuko yake. Hee! Mara meseji ikaingia kwenye simu ya
mume kutoka kwa mtu aliyeseviwa Fundi 1. Meseji yenyewe iliandikwa hivi:
Baby jana usiku nilitamani nikupigie, nikajua utakuwa kwa mkeo. Naomba
basi ile pesa ya pango maana mwenye nyumba ananisumbua sana.” Mke
akapigwa butwaa.
Mara ikaingia nyingine kutoka kwa mtu aliyeseviwa jina la Fundi 3,
iliandikwa hivi: “Siwezi kukuacha, nakupenda kuliko unavyofikiria.”
Kimsingi ziliingia meseji nyingi ambazo zilimchanganya mkewe.
Alipojaribu kuingia inbox na out box akakuta meseji nzito zilizomfanya
yule mama aanguke na kuzimia.
Likawa ni tatizo lingine! Baada ya kupita muda mfupi, mume akazinduka
na kuambiwa kilichompata. Akashangaa sana lakini akaambiwa na mkewe
naye alifika pale na katika mazingira ya kushangaza alianguka.
Mume aliposikia hivyo, akakurupuka na kwenda alipokuwa amelala mkewe
na kuchukua simu yake. Kuangalia akakuta meseji kibao kutoka kwa
michepuko yake na zilikuwa zimesomwa na mkewe.
Mume akajua kimenuka! Mke alipozinduka mume akamuomba msamaha sana na
alipokubaliwa, sasa kabadilika na ameachana na michepuko. Wewe
unayechati na michepuko ukiwa mbali na mwenza wako umejifunza kitu?
Tuwasiliane kwa namba hizo hapo juu.
NA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment