Social Icons

Saturday, 26 September 2015

MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM MUDA HUU, WATUMISHI WA OFISI YAKE WAMLILIA


Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (pichani).


Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais-Utumishi wataendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako mzuri.

-------------------------------------------------------------------
Wakati huo huo mwili wa Marehemu Celina O. Kombani umewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Utaratibu wa msiba unasimamiwa na serikali na ofisi za Bunge. Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. Mola ailaze Roho ya Marehemu 
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili muda huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.


Kwa hisani ya Michuzi Media

No comments: