Social Icons

Tuesday, 26 January 2016

Dk Shein Ashiriki Mazishi ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu Zanzibar.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
D1
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki dua ya kuuombea Mwili wa Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati alipofika nyumbani kwa marehemu fuoni michezani Unguja kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia leo asubuhi.

D2
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Mjane wa Marehemu Ramadhani Nyonje Panda alipofika nyumbani kwao fuoni michezani kutowa mkono wa pole kwa wana familia, kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis.
D3
WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wac Jimbo la Muyuni Zanzibar.
D4
WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakiwa nyumbani kwa marehemu fuoni michezani Unguja wakisubiri taratibu za mazishi ya marehemu kupelekwa kijiji kwao Paje kwa mazishi.
D5
WANANCHI wakisoma hitma ya marehe katika msiki wa fuoni kabla ya kusaliwa kwa ajili ya mazishi kijijini kwao Paje leo asubuhi.
  D7
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi katika kisomo cha hitma ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu, iliosomwa katika msikiti wa fuoni.
D9
WANANCHI wakiitikia dua baada ya kusomwa kwa hitma ya marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati ikisomwa na Shekh Soraga.
D8
WANANCHI wakiwa na jeneza likiwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu kwa ajili ya kusaliwa katika msikiti wa fuoni
D11
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kubeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.
D12
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi na Wananchi wakishiriki katika Sala ya kumsalia marehemu Ramadhani Nyonje Pandu iliofanyika katika msikiti wa fuoni na kuzikwa kijijini kwao Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
(Picha na Ikulu)

No comments: