Social Icons

Monday 25 January 2016

#JUSTIN RAIS DKT MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

 

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

Aidha, baada ya utenguzi  huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu  jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
 
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.Picha Michuzi Jr-MMG


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

RAIS Dk.John  Pombe Magufuli  ametengua  uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Dickson Mwaimu  kwa ajili  kupisha uchunguzi wa sh. Bilioni  179.6 zilizotolewa kwa ajili ya vitambulisho.


Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue  amesema  kutengua uteuzi huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa vitambulisho vya taifa kusimamishwa kazi ambao ni Mkurugenzi wa Tehama ,Joseph Makani , Afisa Ugamvi Mkuu, Rahel Mapande ,Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni  ,pamoja  na Afisa Usafirishaji ,George Ntalima.

Balozi Sefue,amesema kuwa kutengua uteuzi  huo  unatokana na kuwepo kwa malalamiko ambayo yamemfikia Rais juu ya wananchi kukosa vitambulisho vya taifa huku kukiwa na fedha ya Sh.Bilioni 179.6 zikiwa zimetumika .


Rais Dkt Magufuli ameitaka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) ifanye uchunguzi kama kuna vitendo vya rushwa vimefanywa ,amezitaka taasi ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) kufanya uchunguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.


Amesema katika uchunguzi huo CAG ifanye uchunguzi  na kuangalia vitambulisho vya taifa kama vinaendana na fedha iliyotumika ya sh.bilioni 179.6 .


CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP

No comments: