Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amevionya vyama
vya siasa Tanzania Bara na Visiwani kuacha kuzungumzia suala la
mgogogro wa Zanzibar kisiasa kwani suala hilo ni la kiserikali na tayari
linafanyiwa kazi ya utatuzi kwa misingi ya haki za binadamu na sheria
za nchi zinavyoelekeza.
Jaji
Mtungi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
wanahabari na kuwaonya wanasiasa na taasisi mbalimbali kuacha
kuzungumzia mgogoro huo bila kuwa na ushahidi wa baadhi ya hatua
zinazochukuliwa na serikali
Aidha
Jaji Mutungi pia amewataka waandishi wa habari kuacha ushabiki wa vyama
kwa kuandika habari za upande mmoja wa malalamiko kwani zinaweza
kusababisha machafuko na kuhatarisha amani Visiwani Zanzibar.
Na Blogs za Mikoa

No comments:
Post a Comment