Social Icons

Tuesday, 19 January 2016

MHE:BONNAH KALUWA AZINDUA KAMPENI YA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA JIMBO LA SEGEREA.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mwanamitido wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana. Wengine pichani ni mwandaaji wa kampeni hiyo ambaye ni Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa na Mratibu wa Elimu Josephat Peter.
BONA
Mbunge wa jimbo la Segerea,Mhe: Bonnah M.Kaluwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo.BONA1BONA2
Mkutano ukiendelea.

………………
Alichozungumza Mbunge wa Segerea,Mhe Bonnah Kaluwa .

Leo tarehe 17/01/2016,Mimi Bonnah M.Kaluwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Segerea katika wilaya ya Ilala.
Nimekuiteni Asubuhi ya leo ili kuwashirikisha katika uzinduzi wetu wa kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ndani ya jimbo la Segerea,kwakujua dhahiri kuwa ushiriki wa wana habari ni muhimu sana katika kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika jimbo la Segerea na nchi kwa ujumla .
MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ,ni kampeni isiyo na malengo ya kumnufaisha mtu binafsi bali inalenga kuisaidia jamii ndani ya jimbo la Segerea katika upatikanaji wa elimu bora kupitia maboresho ya miundombinu ya shule kama madarasa, vyoo, mifumo ya maji safi na salama, madawati na kadhalika.
Ndugu zangu ninyi wote ni mashahidi kuwa zipo changamoto nyingi katika sekta ya elimu ndani ya nchi yetu zinazohusiana moja kwa moja na masuala niliyoyataja hapo juu.Huku tukilenga kupata;
madawati 15,000,
matundu ya vyoo vya kisasa 1335,
visima vya maji 12, na
vyumba maalum vya watoto wa kike 38.
Kimsingi kampeni hii ni muendelezo wa kampeni iliyowahi kufanyika katika kata ya KIPAWA [ndani ya jimbo la Segerea] kwa kusimamiwa na mfuko wangu wa elimu uitwao BONNAH EDUCATION TRUST FUND mnamo mwaka 2011,kipindi nilipokuwa diwani wa kata hiyo.Kwakuzingatia mafanikio na matokeo chanya ya kampeni hii katika ngazi ya kata;
Kwa moyo wa dhati kabisa, kwakuwa nimechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Segerea ,nimedhamiria kupeleka mafanikio ya kampeni hii kwa kushirikiana na mfuko wangu wa BONNAH EDUCATION TRUST FUND katika ngazi ya jimbo ili basi kila mwananchi ndani ya jimbo la Segerea anufaike na kampeni hii.
Ili kufanikisha kampeni hii, tutawashirikisha wadau mbalimbali wa elimu waliopo ndani na nje ya jimbo la Segerea kama vile Serikali, Makampuni, Mashirika na watu binafsi.
Kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA tunatarajia kuifanya kwa awamu mbili ambazo ni;
Matembezi ya hiyari (Charity walk) na
Chakula cha jioni (Gala dinner).
MATEMBEZI YA HIYARI.
Matembezi haya yatafanyika ndani ya jimbo kwa kushirikisha wananchi ,na wadau wote wa elimu tukiwa na lengo moja tu la kukusanya fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika jimbo letu la Segerea kwa shule za msingi katika kata zote kumi na tatu[13] za jimbo la Segerea.
Matembezi haya yanatarajiwa kufanyika tarehe 25/02/2016, kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 alasiri.
CHAKULA CHA JIONI
Awamu hii ya pili na ya mwisho ya kampeni yetu inatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2016 kuanzia saa 2 usiku na kuendelea.
Katika awamu hii tunatarajia kuwa na chakula cha jioni cha pamoja ambapo wageni kutoka maeneo mbali mbali na nje ya nchi watashiriki nasi katika kuchangia na kuhamasisha upatikanaji wa fedha na mahitaji yote muhimu kuelekea ufanikishaji wa kampeni yetu.
Tunawashukuru ninyi waandishi wa habari na wageni wote waalikwa kwa kushiriki nasi katika uzinduzi huu wa kampeni hii ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA jimbo la Segerea.
Hivyo natangaza rasmi kuwa kampeni hii imezinduliwa rasmi tarehe 17/01/2016.


No comments: