Social Icons

Tuesday 19 January 2016

WENGI WAJITOKEZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
 Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.



SIMANZI, majonzi na vilio vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman aliyefariki dunia leo wakati akiogelea katika bahari ya hindi.


Suleiman alifariki dunia asubuhi akiwa njiani akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan  mara baada ya misuli kukaza ghafla alipokuwa akiogelea.


Ofisa Uhusiano wa TAA, Ramadhan Maleta alisema marehemu huwa anautaratibu wa kufanya mazoezi ya kuogelea kila siku asubuhi kutoka feri hadi Kigamboni.


Alisema leo asubuhi kama kawaida yake alikwenda Feri kwa ajili ya kuogelea saa 12.00 ambapo aliogelea hadi Kigamboni na alipokuwa anarudi  alipata tatizo la kukaza kwa misuli na kuishiwa nguvu.


Maleta alisema mwenzake aliyekuwa anaogelea nae alimuona na kujaribu kumuokoa na kuomba msaada kutoka boti za wavuvi ambao walifika na kumpeleka nchi kavu na kumpa huduma ya kwanza, ambapo alikuwa akiwa njiani kupelekwa hospitali.


Alisema TAA imepata pigo kubwa kwa kupotea kiongozi mahiri ambaye alikuwa hana majigambo wala hakuweka matabaka baina na wafanyakazi na alishirikiana na wote bila kujali nyadhifa zao.


Alisema marehemu alikuwa miongoni mwa viongozi waanzilishi wa kwanza wa TAA mwaka 1999 na atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa na usimamizi wa ujenzi wa viwanja vya ndege vya Songwe na Mpanda.


Pia ujenzi wa awamu ya tatu ta Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julkias Nyerere (JNIA) na viwanja vingine vya ndege vinavyoendelea na ujenzi katika mikoa mbalimbali nchini.


Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliofika nyumbani kwa marehemu walisikika wakilia huku wakisema kuwa TAA wameacha yatima na kwamba pengo la Suleimani ni kubwa kwao na kwa taifa.
  


Kaka wa marehemu, Farid Karamma alisema Suleima atakumbukwa kwa ukarimu wake na alikuwa mtu wa kupenda watu na asiyependa migogoro.


Alisema marehemu ameacha mke mmoja na watoto watatu wa kiume ambao ni Mohammed, Said na Husam Suleima anayesoma katika shule ya sekondari Mzizima Dar es Salaam.


Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani kwake Upanda saa 7.25 mchana ukiwa katika gari la kubebea wagonjwa la msikiti wa Maamur ambapo saa 9.21 ulichukuliwa na kupelekwa msikitini hapo tena kwa ajili ya kuswaliwa, na kisha kwenda kus\zikwa katika makabiri ya Kisutu.
 Mwili ukiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman kabla ya mazishi yake.
 Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman uwasili katika makaburi ya Kisutu leo.
Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
 Waombolezaji.
Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu.
Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu.

 Wadau wa michezo wakibadilishana mawazo. Kutoka kushoto ni Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva, Msemaji wa Simba, Haji Manara, Muhidin Issa Michuzi na Mpoki Bukuku wakibadilishana mawazo wakazi wa mazishi ya aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman. (Picha na Francis Dande)
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments: