Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mbunge
wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) akiwatangazia wananchi na
wanahabari dakika chache zilizopita mara baaada ya Mahakama Kuu ya Ardhi
kusogeza mbele usikilizwaji wa kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa
kwa nyumba za Mabondeni hasa zile zilizopo kwenye bonde la jimbo hilo la
Kinondoni kesi iliyofunguliwa na mbunge huyo kutetea wanachi wake
ikiwemo wapatiwe haki za msingi hasa maeneo mbadala na salama. (Picha
zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Andrew Chale, Modewjiblog
Kesi
ya msingi ya kupinga Ubomoaji wa nyumba zilizopo kwenye mabonde ya
wakazi wa jimbo la Kinondoni iliyofunguliwa na Mbunge wa jimbo hilo,
Maulid Mtulya (CUF) ambayo inataka wananchi hao mbali na kubomolewa
wapewe maeneo mbadala na yenye usalama, iliyofunguliwa Mahakama Kuu
kitengo cha Ardhi, jijini Dar es Salaam, imesogezwa mbele hadi hapo 25
Januari itakapotolewa hukumu.
Akizungumza
na wananchi pamoja na wanahabari, Mbunge huyo, amebainisha kuwa,
baada ya leo Januari 14, kufika mahakamani hapo na pande zote kuendelea
na mashahuriano, ikiwemo Mbunge huyo la kuweka zuio la muda la
kutobomolewa kwa nyumba zote za Mabondeni ndani ya jimbo la Kinondoni,
Hata hivyo waendesha kesi wamesogeza mbele hadi hapo 25 Januari, majira
ya saa nane mchana itakapotolewa mahamuzi kamili.
Awali
nje ya mahakama hiyo iliyopo katikak jengo la Shirika la Nyumba eneo la
Posta, ilijaa na umati mkubwa wa wananchi wa mabondeni wakiwemo wale
waliobomolewa nyumba zao pamoja na waliowekewa alama nyekundu ya X,
wakisubiria hukumu hiyo.
Hata
hivyo baada ya kuharishwa kwa kesi hiyo, wananchi hao walitoa dukuduku
lao kwa Serikali kuchukua hatua ya haraka kumaliza hilikujua hatima yao.
Mkazi
wa mabondeni, Riziwan Mtambo akizungumza na wanahabari baada ya kesi
yao hiyo kusogezwa mbele huku akidai kuwa Serikali inawazunguka kwa
kushindwa kutoa jibu la msingi iliwajue wanachukua hatua gani.
Mmoja
wa wakazi wa mabondeni akizungumza na wanahabari akielezea namna
wanavyopata taabu kila kufika Mahakamani hapo bila kupatiwa jibu la
uhakika. Ambapo aliomba hukumu ya kesi hiyo kutolewa jibu haraka.
Wakazi
hao wakimsikiliza Mbunge wao, Maulid Mtulya (hayupo pichani) wakati wa
kutolewa ufafanuzi wa mwenendo wa kesi yao hiyo iliyosogezwa hadi hapo
25 Januari.
Wakazi
hao wa mabondeni wanaofiuatilia kesi yao ya msingi wakionekana wakiwa
nje ya viunga vya Mahakama hiyo ya ardhi wakisubiria hukumu ambayo hata
hivyo imesogezwa mbele hadi hapo 25 Januari.
No comments:
Post a Comment