Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mkurugenzi
wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya
Idarous Khamsin (katikati) akimtambulisha rasmi mwanadada, Wema Sepetu
(kushoto) ambaye ni miongoni mwa wadhamini wa Jukwaa hilo la Lady In Red
2016. (Kulia) ni Martin Kadinda ambaye naye miongoni mwa watendaji
wanaoratibu jukwaa hilo. Onesho hilo linatarajiwa kufanyika 31 Januari
ndani ya ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady Inn Red fashion show 2016 kama inavyoonekana pichani.
Mwanadada
Wema Sepetu akitoa nasaha zake kwa Wabunifu wa mavazi na wanamitindo
(hawapo pichani) wakati wa utamburisho wa jukwaa la Lady In Red fashion
show 2016 linalotarajiwa kufanyika 31 Januari.
Martin
Kadinda akitoa nasaha zake kwa wabunifu na wanamitindo waliojitokeza
katika mkutano huo (hawapo pichani) kuhusiana na jukwaa la Lady In Red
fashion show 2016.
Wabunifu wa mavazi na wanamitindo wakifuatilia mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.
Baadhi ya wabunifu wa mavazi na mitindo wakifuatilia mkutano huo.
..Wakipata ‘selfie’ na Wema Sepetu
..Wakipata ‘selfie’ na Martin Kadinda
Picha ya pamoja…
Nyota
wa filamu za Bongo, ambaye pia aliwai kuwa Miss Tanzania kipindi cha
nyuma, Wema Issac Sepetu ambaye pia ni mdhamini wa jukwaa la mitindo la
Lady In Red fashion show 2016, Amewataka wabunifu wa mavazi na mitindo
hasa chipukizi nchini kulitumia vizuri jukwaa hilo ili kufikia malengo
yao.
Wema
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano maalum
uliowakutanisha Wabunifu wa mavazi na mitindo kwa lengo la kupanga
mikakati ya ufanikishaji wake hiyo 31 Januari ambapo siku hiyo onyesho
hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni jijini
Dar es Slaam.
Wema
Sepetu amewataka wabunifu hao kuja na utofauti wa kazi zao ambazo
zitakuwa chachu na kivutio kwa watu hiyo itaongeza hali ya kukuwa kwa
tasnia ya mitindo hapa nchini.
Naye
Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red,
Bi. Asya Idarous Khamsin amebainisha kuwa, jukwaa hilo la Lady In Red
litaendelea kuwapo kwani ni shule na daraja la Wabunifu wengi wa mavazi
na mitindo ikiwemo kuibua chipukizi kila mwaka.
“Lady
In Red fashion show 2016 ni ya kipekee na jukwaa hili ni fursa kwa
kuinua wabunifu wa mavazi chipukizi kupata kuonekana zaidi na hata
kukuza majina na ubunifu wao kujulikana ndani na nje” amefafanua Mama wa
Mitindo, Asya Idarous.
Aidha,
ameeleza kuwa, ilikutoa msisimko zaidi kwa jukwaa hilo, siku hiyo
kutakuwa na mambo mbalimbaali zikiwemo ‘surprise’ kutoka kwa watu
maalufu watakaokuwapo usiku huo.
Hadi
sasa jukwaa hilo la Lady in red liimeweza kufikia mwaka wa 12 tokea
kuanziashwa kwake limeweza kutoa wabunifu mbalimbali ambao kwa wengine
wanamajina makubwa akiwemo Ally Rehmtullah, Martin Kadinda na wengine
wengi ambao kwa sasa wamekuwa ni ‘icon’ ya jukwaa hilo.
Pia
Asya Idarous ameomba wadau kujitokeza kuliiunga mkono onesho hilo la
mavazi ikiwemo kudhamini ilikuongeza ukuaji wa tasnia hiyo hapa nchini.
Baadhi ya wadhamini waliopo kwa sasa ni pamoja na Fabak fashions, Wema Sepetu, Super News tv, Modewjiblog na wengine wengi.
Mo Blog
No comments:
Post a Comment