Social Icons

Monday 29 February 2016

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA LA SHINE PHARMACY LA TEMEKE

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog.com
tdfaMmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
Dk KigwangallaNaibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.
wataalamBaadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
dk HK 2Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa duka hilo la Shine Pharmacy , Abraham Mathayo...ambaye alieleza kuwa yupo Mkuranga, hivyo waliamua kuongea naye kwa njia ya simu kwa nini anaendesha duka bila ya kutokuwa na vibali.
Mfamasia wa serikaliMfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
dk hkNaibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo
wakitokaNaibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akitoka katika duka hilo la dawa baada ya kuagiza kulifunga.. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO TV).

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.
Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.
Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.
Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.
Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.
Tazama MO tv, Kuona video hiyo hapa:

No comments: