Social Icons

Tuesday 2 February 2016

fastjet yaongeza ndege ya tano

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje



Dar es Salaam, Januari 28, 2016-Fastjet Tanzania imeongeza ndege nyingine aina ya Airbus A319 kwenye  idadi ya ndege zake nne  na hivyo kuliweka shirika hilo la ndege la gharama nafuu kuendelea na mipango yake ya kupanuka.

“Ndege za fastjet kwa hivi sasa ni nne na zote zinatumika  na ongezeko la ndege ya tano  ni jibu kwenye mikakati yetu ya  kupanuka pamoja na hitaji la kuongeza uwezo wa kubeba kwenye safari zetu za ndani na za kimataifa”, alisema  Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.

Ndege hiyo ya nyongeza  inafanya jumla ya nafasi inayokuwepo kwa siku kwenye safari kwa ajili ya wateja kufikia 1,000.

Fastjet ilianza safari zake nchini mwaka 2012na hivi sasa inajiendesha kwa kutumia ndege tano  aina ya A319 kwenye mtandao wake wa safari ambao unahusisha Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na Zanzibar na kuifanya ijikite kuufanya usafiri wa anga ndani ya Tanzania watu wote waumudu.

Hali kadhalika ilianzisha safari za kimataifa  kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya,  Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli zake.

“Tangu tuanze safari zetu  tumeshabeba abiria zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa  zaidi ya theluthi moja  ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza kumudu  kusafiri kwa ndege”, anasema Corse.

Aliendelea kusema, “kuongeza ndege  nyingine  kwenye safari zetu  kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa  njia zetu zilizopo  ili kukidhi  mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.

Hali kadhalika, Corse anabainisha kuwa  ndege hiyo mpya  inamanisha kuwa fastjet ni sawia na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.

Ndege hiyo A319  ambayo ni Airbus  ni ya injini mbili  ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni nyongeza kwenye  viwango vya juu vya hali ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba  abiria  156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet Tanzania.

Baadhi ya  njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya itakuwa inahudumia  ni njia mpya iliyoanzisjhwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na Nairobi  na Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya  zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye upanuzi wa  njia za fastjet kitaifa na kimataifa.

Fastjet inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya  kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali kadhalika  imeshajionesha kuwa  kuna matarajio ya  kuzindua  safari kati ya Zanzibar na Nairobi  na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.

“Usafiri wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye  kukuza uchumi wa Tanzanoa, hususani kwenye   kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema Corse.

Hali kadhalika Corse alibainisha  kuwa ndege hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za  Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha  kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji  iwapo  ndege moja miongoni mwake  itakuwa haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.

Mwisho








No comments: