Social Icons

Tuesday 23 February 2016

HATARI HII: ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA MOTO MTOTO WAKE AKIMTUHUMU KUKOMBA MBOGA ZA MAJANI AINA YA CHAINIZI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Na  Walter Mguluchuma
   Katavi yetu blog
Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda  linamshikilia   John Noel Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa  Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kumchoma na moto  mtoto wake wa kiume aitwaye Joji Noeri (4(  viganja  vyote  viwili  vya mikono yake na kumuuguza vibaya  na kumsababishia kulazwa Hospitalini  baada ya kumtuhumu  kuwa amekomba  mboga aina ya chainizi
Afisa ustawi wa jamii wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Osca Mkenda aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hilo la unyanyasaji  na ukatili lilitokea hapo juzi katika Mtaa wa Nsemlwa .

Alisema mtoto huyo aliyechomwa na moto na kuungua vibaya  katika viganja vyake vya mikono yake  yote miwili  amelazwa katika  Hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika wodi ya watoto namba 4  na alipokelewa haspitalini hapo hapo juzi.
Baba wa mtoto huyo ambae anashikiliwa na polisi anadaiwa kumchoma na moto  mtoto wake huyo baada ya kumtuhumu kuwa amekomba boga  aina ya chanizi zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajiri ya mlo  wa mchana .
Muuguzi wa wodi hiyo Joseph Mkangwa  alisema hari ya mtoto huyo bado  sio nzuri kutokana na majeraha makubwa  ya moto aliyokuwa nayo ,
 Alisema bado mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu  huku akiwa analelewa na bibi yake mzaa mama yake  aitwaye Hdija Ally  toka alipofikishwa hospitalini hapo.
Bibi wa mtoto huyo  Hadija Ally alisema  mjukuu wake alikuwa akiishi nyumbani na baba yake mzazi baada ya mama wa mtoto huyo  kuwa wameachana na  mume wake hapo mwaka jana .
Alisema  inawezekana  hata mke wake   aliamua kuachana  na kukimbia kwa mume wake kutokana na unyanyasaji kama huo    walipokuwa wakiishi kama mume na mke na baada ya mke kuwa ameodoka ndipo mtoto huyo alilazimika kuishi na baba yake mzazi  ambae amemtendea kitendo hicho cha kikatili na cha kusikitisha .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Mohamed Rashid amekili kutokea kwa tukio hilo na alisema jeshi la polisi linaendelea kumshiklia mtuhumiwa kwa  mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi utakapokuwa umekamilika .

No comments: