Social Icons

Monday 8 February 2016

MAHAKAMA YA TANZANIA YAPOKEA SH. BILIONI 12.3 ZILIZOAHIDIWA NA RAIS.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje






Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga (kushoto) mfano wa hundi wakati wa makabidhiano ya fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju.
 






Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju (kulia) mfano wa hundi wakati wa makabidhiano ya fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga.




Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya fedha zilizotolewa kwa Mahakama leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto).



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju (kulia) akitoa shukrani baada ya kupokea mfano wa hundi aliyopokea kwa lengo la kusaidia mahakama leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.



Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga akitoa shukrani baada ya kupokea mfano wa hundi aliyopokea kwa lengo la kusaidia mahakama leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.



Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao wakati wa makabidhiano ya fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.



(Na. Eleuteri Mangi-Dar es salaam).


Serikali imeikabidhi Mahakama ya Tanzania kiasi cha Sh.bilioni 12.3 zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria kwa lengo la kuiwezesha Mahakama kuimarisha utendaji kazi na kutekeleza majukumu yake inapasavyo.


Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa fedha zilizokabidhiwa kwa Mahakama ni mwitikio wa kutekeleza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani Januari 4, 2016.


“Ni matumaini ya Serikali fedha hizo zitatumika vizuri na zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mpango.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amemshukuru Mhe. Rais kwa kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa ndani ya siku nne na kuudhihirishia umma kuwa kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” anaisimamia kwa vitendo. 


Naye Mtendaji Mkuu wa Mhakama Hussein Katanga amesema kuwa fedha walizokabidhiwa  zitasaidia ujenzi wa mahakama nchini na zipo ndani ya bajeti ya mwaka 2015/2016 na watazitumia kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

No comments: