Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mshindi
wa droo ya pili wa promosheni ya Pasua Anga na StarTimes, Bw. Johannes
Maluli (kulia), akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya kumpata
mshindi wa tatu wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya
Bundesliga. Wakishuhudia katikati ni Balozi wa kampuni hiyo kwa upande
wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda na Meneja Uhusiano
wa Umma, Bw. Muddy Kimwery (kushoto).
Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akimwonyesha mshindi wa droo
iliyopita (ya pili) ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani, Bw.
Johannes Maluli (kulia) na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna
mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga alivyopatikana. Akishuhudia
droo hiyo kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Muddy
Kimwery.
Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na
mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga ya kujishindia safari ya
kwenda Ujerumani. Wakifuatilia kwa makini kulia ni mshindi wa droo
iliyopita Bw. Johannes Maluli na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni
hiyo, Bw. Muddy Kimwery
Balozi
wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za
michezo, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) akimpongeza mshindi wa droo ya
tatu, Johannes Maluli.
Na Dotto Mwaibale
Bi
Kisa Uswege (41) ambaye ni mfanyabiashara wa mchele mkoani Mbeya
amebahatika kuibuka mshindi wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi
ya Bundesliga katika promosheni iliyochezeshwa na kampuni ya StarTimes
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwa njia ya simu Bi. Uswege alisema kuwa amefurahi sana kupata taarifa
hiyo kutoka kwa kampuni ya StarTimes kwani hakutarajia kama angebahatika
kujipatia fursa hiyo.
“Ninafuraha
sana kupokea taarifa hii ya kuambiwa kuwa mimi ni mshindi wa droo ya
bahati nasibu ya tatu ya wateja wanaotakiwa kwenda Ujerumani kushuhudia
mechi ‘Live’. Nashukuru sana kwa ushindi huu kwa hakika nitaitumia hiyo
fursa kwenda Ulaya kushuhudia mechi hiyo. Mimi ninaishi mkoani Mbeya na
ninajishughulisha na shughuli za kuuza mchele, lakini fursa hii pia
ninaimani itanifungulia mambo mengine.” Alielezea kwa furaha Bi. Uswege
“Mimi
ni mteja mzuri wa StarTimes na huwa ninajiunga kila mwezi ili kupata
chaneli na vipindi ninavyovipendelea. Kila mwezi lazima nilipie ili
nifurahie vipindi vyangu au wakati mwingine kwa ajili ya watoto wangu,”
alisema na kumalizia Bi. Uswege kuwa, “Kwa mfano huwa naangalia chaneli
za mipira, filamu za kihindi na kinaijeria. Watoto wangu wao
wanapendelea sana chaneli na vipindi vya Kung Fu, StarTimes Swahili
Bollywood na Novela E1. Kwa mfano hapa nyumbani huwa tunapenda sana
chaneli ya Star Swahili Bollywood kwani filamu zake zimetafsiriwa kwa
lugha ya Kiswahili na kutufanya tuelewe”
Naye
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa kampuni ya StarTimes Tanzania
aliongezea kwa kusema kuwa promosheni hiyo ni ya kweli na haina
upendeleo wa aina yoyote ndiyo maana washindi wanatoka maeneo mbalimbali
zilipo huduma za kampuni hiyo.
“Wiki
iliyopita tulishuhudia mshindi wa droo ya pili akitokea mkoani hapa Dar
es Salaam lakini safari hii ni mama kutoka Mbeya. Promosheni hii
inafanyika kwa kuhusisha wateja wetu wote nchini ukizingatia
atumesambaza huduma zetu takribani mikoa 18 sasa. Ningependa kuwasihi
wateja wetu wazidi kulipia vifurushi vya mwezi kwa kuanzia na kiasi cha
shilingi 5000/- tu na kuendelea na wengine wajiunge nasi kwani kwa
kufanya hivyo watakuwa waeunganishwa na droo hii moja kwa moja.” Alisema
Bw. Kimwery
Kwa
kumalizia Meneja Uhusiano huyo wa StarTimes alisema, “Nawataka wateja
na watanzania kufuatilia droo hiyo ya bahati nasibu kila mwishoni mwa
wiki kwani yeyote anaweza kuwa mshindi. Na pia nawaomba simu zenu ziwe
hewani au kupokea pindi mpigiwapo kwani mnaweza kupoteza bahati.”
No comments:
Post a Comment