Social Icons

Tuesday 16 February 2016

"Nimeandaa mrithi kwa shamba langu, lakini sio kwa Uganda. -Museveni"

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba ameandaa mrithi wa shamba lake lakini sio mrithi wa Uganda na Waganda watachagua mtu wa kuwaongoza pale ambapo yeye atastaafu wadhifa huo.


Museveni ameyasema hayo kipindi ambapo kampeni za lala salama zinaendelea nchini Uganda na uchaguzi wa kumpata Rais wa nchi hiyo unafanyika siku ya alhamisi ya wiki hii.

Rais Museveni ambaye amedumu madarakani kwa muda wa miaka 30 anatetea tena nafasi yake hiyo huku akijitamba kuwa hakuna chama chenye uwezo wa kuweza kushinda chama chake cha National Resistance Movement (NRM)

“Sidhani vyama vya upinzani vitashinda NRM. Kwa sababu tunajua nguvu yetu. Tunajua tutashinda, lakini kama itakuwa tumeshindwa basi tutawaachia wale ambao wameshinda. Lakini sidhani kuna chama kinaweza kushinda NRM wakati huu,” amesema

Aidha kwa sasa katiba inaeleza umri wa juu zaidi wa rais kuwa madarakani ni miaka 75. Kwa sasa Rais Museveni anakaribia kutimiza umri wa miaka 72 maana kwamba mwaka wake wa mwisho wa muhula ujao, iwapo ataingia madarakani, atakuwa na umri wa miaka 76.

No comments: