Social Icons

Monday, 15 February 2016

POLEPOLE ASEMA HAKUNA CHAMA KIZURI KAMA CCM TANZANIA , ASIFU UTUMBUAJIMAJIPU

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Bw Polepole akizungumza leo katika kongamano la shirikisho la wanafunzi wa Vyuo vya juu Iringa , shirikisho la CCM

Polepole akisalimiana na Diwani wa kata ya Nduli Bw Bashir MtoveMkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kushoto akiwa na Kamanda wa Uvccm Mkoa wa Iringa Bw Salim Asas

Na Matukiodaimablog 

MWANAHAKATI Humphrey Polepole amesema chama cha mapinduzi ( CCM) ni chama Chenye misingi ya kweli ya kuwatumikia wananchi ukilinganisha na vyama vingine  asema Kazi ya kutumbua majipu ni nzuri

Huku akiwataka wana CCM jimbo la Iringa Mjini kuanza Kazi ya kueleza mambo mazuri  yanayofanywa na Rais Dr John Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kuwa jimbo la Iringa halikuwa la kwenda mikononi mwa upinzani ataka viongozi wa CCM kujitathimini na kuona wapi walipoanguka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la shirikisho la Vyuo vya elimu ya juu la CCM Mkoa wa Iringa  Bw Polepole alisema kuwa utendaji mzuri wa serikali ya Dr Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM umedhihirisha wazi aina ya wana CCM ambao ni hazina na wanaweza kuleta maendeleo makubwa katika jamii

Kwani alisema kinachofanywa na Rais Dr Magufuli katika kuwatumikia watanzania ni wazi kila Mwananchi anatambua sasa hazina kubwa iliyopo ndani ya chama kwa kutokana na mazuri ambayo Serikali inafanya kazi.

Bw Polepole alisema kuwa ni kweli CCM imepata ushindi katika uchaguzi mkuu uliompa nafasi ya kwenda Ikulu Rais Dr Mahufuli japo alisema ushindi huo wa asilimia 58 bado si mzuri wa kujivunia na kutaka nguvu iongezwe zaidi ili kurudi katika ushindi wa asilimia 80 hadi 88

Alisema kuwa njia pekee ya kuongeza ushindi wa CCM ni lazima kufanya Kazi kukijenga chama na Kazi zake.No comments: