Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Na Modewjiblog team
Uongozi
wa Rais Magufuli unaonekana kujikita zaidi katika kutatua matatizo
yanayowakabili wananchi na kuhakikisha inaboresha huduma wanazopatiwa
wananchi kwa kuwasogezea huduma hizo karibu zaidi.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
ameeleza mpango wa serikali kujenga maabara za wakala wa mkemia mkuu wa
serikali kwa kanda zote nchini.
Mhe.
Mwalimu aliyasema hayo wakati wa makabidhiano ya gari la huduma za
dharura (ambulance) la kituo cha kitaifa cha kuratibu matukio ya sumu
zinazofanyika wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali na kueleza
kuwa serikali inataka kufanya ujenzi huo ili kuwasogezea wanachi huduma
kwa ukaribu zaidi.
“Serikali
kupitia wizara yangu imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha huduma za
wakala kulingana na uwezo uliopo ili kuhakikisha kuwa wakala unaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,
“Baadhi
ya jitahada hizo ni pamoja na, kuanzisha maabara za kanda ili kusogeza
huduma karibu na wananchi na kuendeleza ujenzi na ukarabati wa majengo
ya wakala,” alisema Mhe. Mwalimu.
Aidha
Mhe. Mwalimu alisema tayari wizara yake imeshapeleka muswada bungeni
ili bunge litunge sheria ambayo itampa wakala uwezo wa moja kwa moja
kisheria kufanya kazi na kutekeleza majukumu kwa uhakika na ufanisi.
Pia
Waziri wa Afya amewataka wananchi na taasisi mbalimbali kuiamini
maabara hiyo kwa kuitumia kufanya vipimo wanavyohitaji bila kuwa na
mashaka.
Hata
hivyo katika maadhimisho hayo, Mhe. Ummy Mwalimu alizindua cheti cha
Ithibati (Accreditation ISO 1705:2005) ambacho kinaifanya maabara hiyo
kutambulika kimataifa.
No comments:
Post a Comment