Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya
unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa
Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa
mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa
utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni
Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini
Tanzania.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE
Carol
Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania
akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Dk.Ulisubisya
Mpoki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto akichangia hoja katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.
Dk.
Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika
mkutano huo ambao umekutanisha wadau wa afya na kujadili changamoto
mbalimbali zinazokabili sekta ya afya.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa
tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya
afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa
tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya
afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
........................................................................................................................
TAMKO LA PAMOJA KUHUSU VIPAUMBELE VYA SEKTA YA AFYA KWA MWAKA 2016/2017
- KINGA NA AFYA YA JAMII
Mwaka
2015 Serikali ya Tanzania ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na
kuanzisha mafunzo kwa kada mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community
Health Workers). Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii
huduma za afya za msingi.
Mwaka 2016, Serikali ya Tanzania itaendelea kutekeleza agenda ya
huduma za Afya katika jamii kwa kuhakikisha ubora wa mafunzo kwa
wahudumu wa Afya ya Jamii, kuendelea kuajiri wahudumu wa Afya ya Jamii
na kufikisha huduma za Afya za Kinga na tiba karibu zaidi na jamii.
- UWIANO
Mpango
Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya (HSSP IV) umejielekeza zaidi katika
uwiano na kusaidia maboresho katika Sekta ya Afya katika maeneo ya
pembezoni ambayo huduma za Afya hazifiki kwa urahisi. Jambo muhimu
katika hili ni kuendelea kusambaza kwa uwiano rasilimali zote za
kifedha zilizopo kutoka vyanzo vya ndani na nje.
Ili
kuhakikisha uwiano katika mgawanyo wa rasilimali, ni muhimu kuwa na
takwimu sahihi kuhusu uwepo wa rasilimali kutoka vyanzo vya nje hususan
wadau wa maendeleo, sekta binafsi, mashirika ya dini na mashirika yasiyo
ya kiserikali katika ngazi ya wilaya.
Serikali
itahakikisha kwamba takwimu zilizopo zinaboreshwa kwa kukamilisha
Mpango Kabambe wa kutambua vyanzo vya nje vya mapato kwa mwaka 2016.
- UGHARAMIAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Mpango
wa Afya kwa wote ni kipaumbele cha Serikali ya Tanzania. Mkakati mpya
wa ugharamiaji wa Afya ulioandaliwa umeweka wazi njia ambayo Tanzania
inaweza kutoa huduma za Afya za uhakika wa kifedha kwa raia wote
kupitia mfumo mmoja wa Bima ya Afya ya Taifa.
Kwa
mwaka 2016/2017, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto itatafuta kibali kutoka Mpango Mkakati wa ugharamiaji Afya na
itaandaa hatua muhimu za utekelezaji wa Mkakati ikiwa ni pamoja na
kuhamasisha kupitishwa kwa Sheria ya Mfuko Mmoja wa Kitaifa wa Bima ya
Afya na kuleta pamoja mitazamo mbalimbali ya Mfuko wa Afya ya Jamii.
Vilevile,
wizara itafanya uhamasishaji ili kuongeza rasilimali za ndani kwa ajili
ya Sekta ya Afya na kuongeza jitihada za Wizara mbalimbali katika
kuboresha matumizi yenye ufanisi wa rasilimali fedha zilizopo.
Wizara
na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zitaunda Mfumo
rahisi wa utoaji taarifa kuhusiana na mipango, bajeti na fehda, kwa
ajili ya vituo vya utoaji huduma za afya, ili kuwezesha ugatuaji wa
kifedha kutoka wilaya kwenda ngazi ya vituo vya afya.
- UTAWALA NA UONGOZI
Kuna
miundo mbalimbali ya utawala na uwajibikaji ndani ya Serikali na katika
jamii inayofanya kazi katika ngazi ya wilaya hususani katika masuala ya
Afya kama vile Kamati za Uongozi za Vituo vya Afya na zile zenye
mamlaka makubwa zaidi kama vile Kamati za Maendeleo za kata. Zote hizo
zinajukumu la kuhakikisha uwajibikaji katika utoaji huduma za Afya kwa
wananchi.
Kwa
mwaka 2016 Wizara, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
na Wadau wengine zitaweka wazi mahusiano kati ya miundo hii katika ngazi
ya wilaya kuhusiana na Usimamizi wa Mipango, bajeti na fedha kwa ajili
ya Afya. Vilevile ili kuendeleza agenda ya ugatuaji, Wizara
itashirikiana na Wizara ya Fedha kusimamia mgawanyo wa fedha katika
ngazi ya vituo vya kutolea huduma za Afya.
- RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA AFYA.
Kuvutia
na kuwezesha idadi kubwa ya watumishi kuendelea na kazi katika utoaji
huduma bora za Afya hususan katika maeneo ya vijiji na maeneo ambayo
huduma za Afya hazifiki kwa urahisi, ni changamoto nchini Tanzania,
maendeleo ya kuridhisha yamefanyika kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa
Sasa na Program nyingine.
Ili
kuendeleza zaidi mafanikio yaliyofikiwa, mwaka 2016 Wizara, Ofisi ya
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa zitaendeleza Sera ya mabadiliko yanayohitajika ili
kutekeleza mpango wa mabadiliko makubwa sasa (BRN) kuhusiana na
rasilimali watu katika nyanja za afya na zitashirikiana na Serikali za
Mitaa kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Malipo na motisha.
Ili
kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya, Wizara itakamilisha
mwongozo wa kushirikiana katika majukumu, kuweka wazi majukumu ya kila
kada na kukamilisha mwongozo wa kujiendeleza kitaaluma.
- DAWA, VIFAA NA VIFAA TIBA
Uboreshaji
wa usimamizi na utawala wa Dawa, vifaa na vifaa tiba katika vituo vya
kutolea huduma za afya hususan katika ngazi ya wilaya ni kipaumbele
chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa na Mpango wa Nne wa HSSP.
Matatizo
ya kifedha yana maanisha kwamba rasilimali zilizopo hazina budi
kutumiwa kwa ufanisi na namna nyingine za ugharamiaji wa dawa na vifaa
vingine muhimu hazinabudi kutafutwa. Ili kuhakikisha haya yanafanyika,
mwaka 2016 Wizara itajielekeza katika kuboresha utendaji na ufanisi wa
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ikiwa ni pamoja na kuwezesha ulipaji wa deni.
Kwa
kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Wizara vilevile itahakikisha rasilimali zilizopo na nyingine mpya kwa
ajili ya usambazaji wa vifaa zitaelekezwa katika vipaumbele vya mpango
wa Matokeo Makubwa Sasa na itatoa miongozo sahihi ya Kisera inayoainisha
Mfumo mmoja wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba muhimu itakayofuatwa na
mamlaka ya Serikali za Mitaa na vituo vya kutolea huduma za Afya.
- UFUATILIAJI, TATHMINI NA USIMAMIZI WA TAKWIMU
Maboresho
mengi yamefanywa katika mfumo wa usimamizi wa takwimu kwenye Sekta
katika miaka ya hivi karibuni, hata hivyo bado kuna changamoto hususan
kwa upande wa uhamiaji kwenda katika Mfumo wa kielektroniki na matumizi
ya takwimu katika utoaji wa matumizi.
Uwepo wa takwimu sahihi utasaidia wilaya kupanga vizuri matumizi yao.
Wizara
imedhamiria kukamilisha Mpango wa kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya
huduma za afya kufikia mwisho wa mwaka 2016, ikiwa ni pamoja na
kuhama kutoka mfumo wa kutumia karatasi kwenda mfumo wa kielektroniki na
pia katika kuongeza uwezekano wa kuunganisha mifumo ya takwimu.
Ili
kuendeleza dhana ya utoaji uamuzi unaotokana na ushahidi, Wizara
itashirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
katika masuala ya takwimu muhimu zinazotokana na mamlaka za Serikali za
Mitaa na watumiaji wengine kwa wakati katika mfuko rafiki unaowezesha
utoaji wa taarifa za mipango na utoaji wa maamuzi.
- UTOAJI HUDUMA
Mwaka 2015 Wizara ilianzisha Mfumo wa tathmini wa vituo vya msingi vya utoaji huduma za afya.
Mfumo
nyota ambao unazingatia vigezo vya ubora wa huduma (quality of service)
za madaraja katika kuanzisha viwango vya utoaji huduma. Mwaka 2016
Wizara kwa ushirikiano na TAMISEMI itahakikisha kwamba tathmini ya
Matokeo ya nyota inatafsiriwa katika uboreshaji huduma katika vituo na
kwamba ugharamiaji unawekwa katika Mpango Kabambe wa Afya wa kituo na
Halmashauri. Mfumo nyota unaonyesha vituo katika kazi mkoa, rufaa na
Taifa utakamilika 2018.
Vilevile, Wizara itaipitia miongozo iliyopo ya usimamizi ili kuainisha majukumu ya ukaguzi na usimamizi.
UZINDUZI WA MPANGO MKAKATI WA NNE WA SEKTA YA AFYA 2015-2020
Utangulizi
Mpango
mkakati wa nne (HSSPIV) ni mpango ulioandaliwa kwa kuwashirikisha wadau
wote wa sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na Serikali, Wadau wa Maendeleo,
Sekta binafsi, taasisi za kijamii na Ustawi wa jamii.
Lengo kuu la mpango huu ni :kufikisha huduma bora muhimu za Afya na Ustawi wa jamii katika ngazi za kaya zote nchini.
Mpango unaainisha Mikakati mitano:
1.Kuboresha
kiwango cha Ubora wa huduma katika ngazi zote za afya ya msingi kwa
kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na kitita bora cha afya na
ustawi wa jamii
- Kuboresha Uwiano wa upatikanaji wa huduma bora za afya na ustawi wa jamii kwa kuondoa tofauti zilizopo za kijografia, kiuchumi na makundi maalum kama vile wazee, watoto, wajawazito na walemavu.
- Kuboresha Ushirikishwaji wa jamii katika kupanga na kusimamia huduma za Afya na Ustawi wa jamii. Hii inajumuisha uhamasishaji wa mifuko ya afya ya jamii, usimamiaji wa vituo vya huduma, uwepo wa dawa vituoni, utambuzi wa wasiojiweza ili wapate huduma, na uwajibikaji wa watoa huduma kwa wanajamii husika.
4.Uwekezaji katika mikakati na njia za kisasa na ubunifu
kama : Ugharamiaji
-Mkakati wa Bima moja ya Afya kwa wote
-Ushirikiano na sekta binafsi
-Ushirikiano wa wadau wote wa sekta ya afya maendeleo na ustawi waj amii.
5.Kutambua
Ushiriki wa jamii na Sekta nyingine katika afya. Afya bora siojukumu la
wizara moja; Hii inajumuisha uhamasishaji wa wa kila sekta kuwa na
mkakati wa Afya. Hii itasaidia kushughulikia mambo muhimu kama; Lishe
na afya za watoto, Maji safi, elimu ya afya, Usafi wa mazingira,
umuhimu wa barabara na mawasiliano katika dharura ya kiafya na
itapunguza magonjwa kama kipindupindu, vitambi, presha
No comments:
Post a Comment