Social Icons

Tuesday 9 February 2016

SERIKALI YASEMA ITAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA YA NCHI RAFIKI NA WADAU WA MAENDELEO ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI NA KUPUNGUZA UMASIKINI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

 Na Magreth Kinabo-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea kudumisha na   kuimarisha mahusiano ya kideplomasia kati ya nchi rafiki na wadau wa maendeleo ili kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kutimiza malengo ya Mpango wa Maendeleo Endelevu wa Milinea (MGDs) ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni hatua ya  kuhakikisha inapunguza kiwango cha umasikini na kuboresha maisha ya watu nchini.


Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na  Kimataifa,  Balozi Dkt. Augustine  Mahiga kwa niaba ya Rais wa  Jamhuri ya   Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 iliyoshirikisha mabalozi mbalimbali wanazoziwakilisha nchi zao hapa nchini iliyofanyika leo jioni Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Hivi sasa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Bara umekwisha. Ni wakati wa kufanya kazi na kauli mbiu yangu ni “Hapa Kazi Tu”. Serikali mpya ya Awamu ya Tano imekuja na mkakati wa kuboresha na kuimraisha utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ili kusisitiza nidhamu na utendaji kazi, kuhesimu haki za binadamu, utawala bora na kuhakikisha  wananchi wote wa Tanzania wanapata  maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii,”alisema Balozi Mahiga.

Balozi Mahiga aliongeza kwamba Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameiacha nchi ikiwa imara na marafiki wengi, pia uchumi wake umekuwa katika kiwango cha asilimia saba (7) kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi za ushirikiano na misaada yao, hivyo aliwashukuru kwa michango yao waliyoifanya hapa nchini.
“Ninawaomba muendelee kutusaidia kwa kuwa hivi sasa tuna mipango ya maendeleo ambayo ina lenga kuboresha maisha ya Watanzania wote hususan wale wanaoishi katika kiwango cha chini cha umasikini,”alisema Balozi Mahiga.

Alizitaja changamoto kubwa zilizopo katika kutimiza malengo hayo ni kuwepo kwa hali ya umasikini nchini, ukosefu wa ajira na rushwa. Hivyo Serikali inafanya kila jitihada za kukabiliana na changamoto hizo kwa kuwa bila ya kufanya hivyo itakuwa ni vigumu kutimiza malengo ya nchi ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Balozi Mahiga alisema kwamba ili kutimiza malengo hayo, Serikali hivi sasa inaendelea kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali, kujenga nidhamu, uwazi na uwajibikaji katika matumizi hayo ndani ya Serikali na hata kwa sekta binafsi na kuimarisha maeneo ya ukusanyaji wa mapato.

Aidha, Serikali imesema kwamba itaendelea kuendeleza ushirikiano huo, ili kuweza kupambana na vitendo vya rushwa, biashara haramu ya binadamu, ugaidi na matumizi ya silaha.
“Tunawaomba mtusaidie husasan kwenye eneo la upatikanaji wa taarifa, kujenga uwezo na masuala ya kiufundi katika kukabiliana na vitendo hivi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu suala la Uchaguzi wa Zanzibar, Balozi Mahiga alisema Zanzibar inajitegemea katika masuala ya kisiasa na kiutamaduni licha ya kuwa ni sehemu ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Mahiga alifafanua kuwa Zanzibar ina Katiba yake, Serikali na Tume Huru ya Uchaguzi .Hivyo kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 ulifutwa kwa sababu mbalimbali kama  ilivyoelezwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).
Aliongeza kwamba mazungumzo   ya kufikia muafaka wa suala hilo, yanaendelea ma uchaguzi mwingine utafanyika Machi 20, mwaka huu. Hivyo mazungumzo hayo bado yanaendelea ili kuufanya uchaguzi huo uwe huru, haki na uwazi ili kukidhi viwango vya kimataifa vya demokrasia.
 

No comments: