Social Icons

Tuesday, 9 February 2016

Waziri Dkt. Mahiga akutana na Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Mabalozi na Wadau wa Maendeleo wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2016 leo Ikulu jijini Dar es salaam.

 

Kiongozi wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania Balozi wa Zimbabwe nchni Tanzania Idzai Chimonyo akitoa shukrani kwa niaba ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2016 leo Ikulu jijini Dar es salaam.


Baadhi Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania wakifurahia jambo wakati wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2016 leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Baadhi Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2016 leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na Wawakilishi wa Wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini Tanzania wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2016 leo Ikulu jijini Dar es salaam.

(Picha na Eleuteri Mangi)


No comments: