Social Icons

Monday 22 February 2016

UINGEREZA YAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

RAIS DK.MAGUFULI
Uingereza Imempongeza Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli Kwa Jitihada Zinazofanywa Na Serikali Yake Katika Ukusanyaji Wa Mapato Na Kukabiliana Na Vitendo Vya Rushwa.

Akizungumza Baada ya Kukutana na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo, Balozi Huyo, Dianna Melrose Amesema Juhudi za Mapambano dhidi ya ufisadi pamoja na kubana matumizi na ubadhirifu wa mali za umma kunakotekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya Tano ni mfano wa kuigwa.


Balozi Melrose amesema Waziri Mkuu wa nchi ya Uingereza, David Cmeroon amevutiwa na Utendaji kazi wa Rais Magufuli na kusisitiza kwamba nchi hiyo itaendeleza ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Uingereza na Tanzania Katika Nyanja Mbalimbali Za Maendeleo.

Kabla Ya Kukutana Na Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini Rais Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Afrika Ya Kusini Hapa Nchini Mh Thamsanqa Mseleku,Na Balozi Wa Misri Hapa Nchini Mh Mohamed Yasser El Shawaf Ambao Amewahakikishia Kuwa Serikali Yake Ya Awamu Ya Tano Itaendeleza Ushirikiano Mzuri Uliopo Kati Yake Na Nchi Hizo Hususani Katika Kukuza Biashara Na Kuwanufaisha Wananchi Wa Pande Zote.

Katika Hatua Nyingine Rais Magufuli Amepokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wawili.

Mabalozi Waliokabidhi Hati Zao Za Utambulisho Ikulu Jijini Dar Es Salaam Ni Mh Jean Pierre Mutamba Tshampanga Wa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Mh Theresia Samaria Wa Namibia.

Rais Magufuli Amewaeleza Mabalozi Hao Kuwa Tanzania Itaendelea kushirikiana Na Nchi Hizo Katika Nyanja Mbalimbali Hususani Katika Uchumi.

Wakati Huo Huo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

No comments: