Social Icons

Monday 22 February 2016

Bodi TSN yamsimamisha kazi Mhariri Mtendaji.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN leo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye akiongea na vyombo vya Habari kuhusu maagizo aliyoyatoa kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya serikali TSN ikiwemo sababu za wafanyakazi wengi kuacha kazi katika shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba(wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki(hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi hiyo Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitembezwa kuonyeswa mazingira ya kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni mhariri mtendaji wa kampuni hiyo ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki ambaye amesimamishwa kazi kutokana na utendaji usiorizisha na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba. Picha na Daudi Manongi.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mchapaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN) Bw.Paul Kasele alipofanya ziara katika shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.


Bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.

“Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.

Aidha Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.

Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21 kuacha kazi.

“Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.

No comments: