Social Icons

Wednesday 3 February 2016

VIPIMO VYA MAGONJWA YA DARATANI KUTOLEWA BURE

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani .
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habarileo jijini Dar es salaam  kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani.
Picha na Ally Daud

Na Nyakongo Manyama



Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wanatarajia kutoa  elimu, huduma na vipimo vya  bure vya magonjwa ya saratani ili kuiwezesha jamii kujikinga na ugonjwa huo nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatano) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa  Wizara hiyo, Dkt. Ulisubisya Mpoki huduma hizo za matibabu na vipimo vitaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya saratani duniani inayoathimishwa ulimwenguni kote tarehe 4. Februari ya kila mwaka.

Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza Dkt. Mpoki.

Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI.
 

No comments: