Social Icons

Wednesday, 24 February 2016

WATAKA KUANDAMANA KUPINGA ENEO LAO KUCHUKULIWA NA KAMPUNI YA MZINDAKAYA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

   Na Walter Mguluchuma
      Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  amevuia  kufanyika kwa maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu   katika Kijiji cha Dilifu Kata ya Magamba  Wilayani hapa waliotaka kuandamana kupiga   kuzuiwa  kunya shughuli katika eneo hilo  na kupewa kampuni ya  JANI  INVESMET Inayomilikiwa na mwanasiasa mkongwe Crisanti Mzindakaya.

Wachimbaji hao wadogo wa madini ya dhahabu walikuwa wamepanga kufanya maandamano hayo hap oleo yaani jana  kuanzia katika eneo hilo la Dilifu hadi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda umbali wa kilometa  13  kwalengo la kupinga  uamuzi wa wizara ya Nishati na madini  Kanda ya magharibu kwa uamuzi wake wa kuwataka wachimbaji hao kusitisha  shughuli zao za uchimbaji katika eneo hilo na  ipisha kampuni ya JANI INVESTMENT  mali ya Mzindakaya.
Mkuu huyo wa  Wilaya alilazimika  hapo jana kwenda katika eneo hilo la Kijiji cha Dilifu na kufanya mkutano wa hadhara  ilikuweza kuwasikiliza wachimbaji hao wadogo ambao walianza kujikusanya katika eneo hilo toka saa  kumi na mbili asubuhi kwa ajiri ya kusubili mkutano huo wa hadhara.
Diwani wa Kata hiyo Philipo Kalyalya alieleza kuwa  alieleza kuwa  wachimbaji hao wadogo  hao wapatao 2300 wanataka kupata ufumbuzi wa tatizo hilo  kwani maisha yao ya kila siku   yanategemea uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoa wa Katavi Wiliy Mbogo alisema kuwa  wachimbaji wadogo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maeneo  kutoka na Wizara ya Nishati ya Madini kutowatengea maeneo ya kuchimba wachimbaji wadogo kama ambavyo sheria ya madini inavyoeleza.
 Alisema matokeo yake wizara hiyo imewapatia eneo wachimbaji wadogo katika eneo la Kijiji cha Kapalamenga  yanakopatikana madini aina ya kopa wakati wachimbaji wengi wa madini wa Mkoa wa Katavi wanachimba dhahabu .
Mwenyekiti wa kitongoji cha Dilifu  Ismaili Idd alieleza kwenye mkutano huo ambao wachimbaji walionekana kuwa na hasira kuwa eneo hilo ni  eneo halali la Kijiji hivyo wawekezaji wanatakiwa kufuata taratibu .
 Alisema  hapo awali waliambiwa na Wizara ya Madini kanda ya magharibi kuwa  eneo hilo wanalofanyia shughuli za uchimbaji ni eneo la kampuni ya uchimbaji ya madini ya GBA  ambayo wao haajawahi kuiona hata siku moja kampuni hiyo .
Mwenyekiti huyo wa Kitongoji alieleza juzi walishangazwa na agizo kutoka Wizara ya madini kanda ya magharibi ikiwataka kuanzia  leo yaani jana kusitisha shughuli zao za uchimbaji kwa kuwa eneo hilo wapewa kampuni nyingine inayoitwa JANI INVESTMENT  inayomilikiwa na  Crisanti Mzindakaya  ndipo wachimbaji baada ya kupata taarifa hizo waliamua kufanya maandamano ya kupinga kwa kampuni hiyo kupewa maeneo.
Mussa Mkana mchimbaji mdogo alieleza kuwa  karibu maeneo yote ya uchimbaji wa madini kila wanapohitaji kupatiwa maeneo hayo wamekuwa wanaambiwa kuwa yameisha chukuliwa na wachimbaji wakubwa KIJANI   INVESMENT    hata hivyo maeneo hayo yamekuwa hayaendelezwi.
Daudi Sumuni alisema  kikubwa wachimbaji wadogo hawaitaki kampuni hiyo kufanya shughuli kwenye eneo hilo na wao hawako tayari kuiona  kwenye machimbo hayo ya dhahabu .
Kaimu Meneja wa madiwa wa kanda ya magharibi  mhandisi    Giliard Luyoka  aliwataka wachimbaji hao wadogo kufanywa shughuli zao kwa kufuata sheria za uchimbaji wa madini .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  aliagiza wachimbaji hao wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji  na sikama walivyokuwa wamezuia kufanya shughuli hiyo  na akawahidi kurudi baada ya siku saba ilikuwapatia maekezo yatakayo kuwa yametolewa na waziri wa nishati na madini .
 Alisema serikali inawahitaji sana wawekezaji  lakini wafuate sheria  na pia alisema yeye kama mkuu wa Wilaya hiyo  haja pata taarifa yoyote ya kampuni hiyo kuomba eneo hilo

No comments: