Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Bw. Omar Jumanne Bakari (wa
tatu kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda
Vidogovidogo (SIDO) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya
Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa
Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika
kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es
Saalam na mikoa ya jirani.
Bibi.
Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (wa tatu
kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Mjuli Mkurugenzi Mtendaji,
kuhusu utengenezaji wa batiki katika moja ya viwanda vidogo vinavyofanya
kazi chini ya mwamvuli wa SIDO. Wengine pamoja nae ni wataalam kutoka
Tume ya Mipango na SIDO.
Bibi.
Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, pamoja na timu ya maofisa
kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu Bw.George
Buchafwe kuhusu utengenezaji wa mazulia kwa kutumia malighafi
zinazopatikana hapa nchini.
Bibi.
Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (wa pili kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Bw. Obedi Sylvester Musiba Mkurugenzi wa
kampuni, (wa kwanza kushoto), kuhusu bidhaa wanazotengeneza kutokana na
mimea na matunda. Wengine ni Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu
SIDO (wa pili kushoto), Bw. Omary Abdallah, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya
Mipango na Ufuatiliaji (wa tatu kushoto), pamoja na maofisa kutoka Tume
ya Mipango.
Viongozi
na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw.
Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa
vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
Viongozi
na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya
kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika
kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile.
Bibi.
Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, alipata pia
fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa
mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na
matoroli (wheelbarrows).
Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO
(aliyesimama), akitoa maelezo kwa viongozi na maofisa kutoka Tume ya
Mipango (waliokaa kushoto) kuhusu SIDO inavyofanya kazi katika
kuwasaidia wazawa ili kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo.
Waliokaa kulia ni wamiliki wa viwanda vidogovidogo wanaofanya shughuli
zao chini ya SIDO.
Na: Thomas Nyindo
Tume ya Mipango
No comments:
Post a Comment