Social Icons

Monday, 15 February 2016

Waziri wa Afya awasimamisha wakurugenzi wanne MSD

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
 
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Waziri wa Afya ,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amewasimamisha wakurugenzi toka Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD) kwa ubadhilifu wa fedha takribani Shillingi Billion 1.5.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kupokea  vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) amesema amepata taarifa ya uchunguzi ofisini kwake ya ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha na kuamua kuwasimamisha wakurugenzi wanne kupisha uchunguzi.

“ Nimepata taarifa toka ofisini kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa,nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe.Rais kwahiyo  nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi”

“ Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo  ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.

Amewataja aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa kuwaandikia barua mara moja ya kuwasimamisha kazi.

Katika kuboresha sekta ya afya nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi  kwa taratibu na misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya hasa katika sekta ya afya kwa ujumla.

No comments: