Social Icons

Tuesday 15 March 2016

BILLIONI 12 ZAKUSANYWA KUTOKA KWA WAKWEPA KODI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO
15/3/2016. Dar es salaam.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya takribani Sh. billioni 12 kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikwepa kodi na kupewa muda wa siku 14 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli kulipa kodi hizo kwenye mamlaka hiyo.

Akitoa takwimu hizo mara baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amesema, kila Mtanzania ana jukumu la kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na sio kukwepa na amehaidi kulisimamia vizuri suala la ukusanyaji wa mapato katika sehemu mbalimbali ili kuongeza mapato ambayo yatasaidia kufanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali.

“Tutajitahidi kwa kila namna kuwaelimisha wananchi wetu ili wafahamu wajibu wao na umuhimu katika kulipa kodi na sio kukwepa kulipa kodi na tunawaomba wananchi kila waendapo kupata huduma yoyote ile iwe katika sekta binafsi au Serikalini  basi anatakiwa aombe stakabadhi za manunuzi au huduma ili tuweze kudhibiti upotevu wa kodi” alisema Kidata.

Kamishna  aliongeza kwamba Kidata mamlaka hiyo ipo kwa ajili ya  kuwahudumia wananchi na kama kuna suala lolote au tatizo kuhusu kodi kuna ofisi katika mikoa yote ikiwa ni hatua ya kutatua shida zao na kama kuna mtumishi yoyote wa mamlaka hiyo atashindwa kumuhudumia mwanachi inavyotakiwa basi taarifa zitolewa mara moja kupitia namba zao zilizoko kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, ambayo ni www.tra.go.tz ili kuimarisha huduma zetu kwa wateja.

Aidha Kamishna Mkuu huyo amesema kuwa watawachukulia hatua wale wote ambao hawatalipa au hawajalipa kodi zao kwa kuwapeleka mahakamani kwa kukaidi kulipa kodi halali kwa mujibu wa Sheria.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na ina mamlaka ya usimamizi wa makusanyo ya Mapato Tanzania na kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ukwepaji wa kodi uliotokana na sakata la upotevu wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo kuikosesha mapato Serikali lakini jitihada thabiti zimefanywa na mamlaka hiyo kukusanya madeni kutoka kwa wakwepa kodi na kuwafikisha mahakamani ambao wamekaidi kulipa.



No comments: