Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;
Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, James
Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya matumizi ya jiko
linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa Tanzania Agriculture
Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya
kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya
Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;
Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, James
Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya kilimo cha mbogamboga toka
kwa Mwenyekiti Kinondoni Saccoss Neema Urio (Kulia) katika ufunguzi
mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kulia mwa Mkurugenzi Maendeleo
ya Vijana ni Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga
na kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Uratibu, Bunge,
kazi, Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, James Kajugusi (mwenye koti la
Draft) akitoa ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring
wa Sinza Dar es Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali
yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji
Idara ya Vijana Esther Riwa.
Mkurugenzi
Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki
(hawapo pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana
yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga akiongea na washiriki
wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana taifa James Kajugusi.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri
Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu James
Kajugusi akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa mafunzo ya kilimo
cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya vijana wakimsikiliza mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo
cha kisasa kwa vijana katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na
kushirikisha vijana toka Dar es salaam na Pwani.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John
akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo
hayo yanayofanyika kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri
Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James
Kajugusi akipongezana na Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana
Venerose Mtenga mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya kilimo cha
kisasa kwa vijina yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri
Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James
Kajugusi akisalimiana na Mwenyekiti wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa
vijana Bi Mary Lucian Mdendemi mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya
kilimo cha kisasa kwa vijina yanayofanyika jijini Dar es Salaam,
katikati ni Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa. (Picha
zote na Raymond Mushumbusi – Wizara ya Habari).
Katika
kuboresha na kuongeza ajira hapa nchini serikali imeahidi kuwapatia
vijana mtaji na maeneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa ili waweze
kujiendeleza na kukuza kipato chao.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha “Green Houses”
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu,
Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi
amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa mbalimbali
zinazojitokeza katika kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.
Ameongeza
kuwa serikali inaendelea kuwawezesha kupata mikopo kwa riba nafuu na
kutoa elimu kuhusu kilimo bora cha kisasa ili kuondoa fikra zilizopo
kwa vijana kuwa kilimo ni kwa ajili ya watu waliokosa elimu, wenye
maisha duni na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Ni
lazima tutumie fursa zinazojitokeza katika kunufaika, nina imani
mtatumia fursa hii kwa manufaa yenu na elimu mtakayopata itawasaidia
kuzalisha bidhaa bora na kuondoa utegemezi,” alisema Mkurugenzi
Kajugusi.
Aidha
mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw Praygod Mushi amewataka vijana hao
kuamini kuwa kilimo kinaweza kubadilisha maisha yao kama watatumia
fulsa zote zinazojitokeza katika sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya
familia mpaka taifa.
Naye
mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bi. Jasmini John ameishukuru
serikali kwa kuaandaa mafunzo hayo na kusema kuwa atatumia elimu
atakayopata kuendeleza kilimo kama ajira kwa kutumia pembejeo za kisasa
atakazoelekezwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo
ambayo vijana hao wamepewa ni jinsi ya kutumia dawa na mbegu bora
katika kilimo,kunufaika na mazao yatokanayo na kilimo cha Green House,
utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati ya mwanga wa jua pamoja na
ubunifu wa shughuli za vijana katika jitihada za kukuza viwanda kwa
kutumia mali ghafi za humu nchini.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu kuanzia leo na yameshirikisha vijana kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Na Shamimu Nyaki.
No comments:
Post a Comment