Social Icons

Tuesday, 1 March 2016

WADAU WA MFUKO WA LAPF KUKUTANA ARUSHA MACHI 10-11

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Valerian Mablangeti akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari muliofanyika leo jijini Dar es Salaam nane, kuhusu mkutano wa 8 wa wadau wa mfuko huo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 10-11. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe. (Picha na Francis Dande).
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua jambo jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa nane wa wadau mfuko huo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 10-11. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa nane wa wadau mfuko huo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 10-11. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti. NA MWANDISHI WETU

JUMLA ya wanachama 246 wamefaidika na mkopo wa upimaji ardhi ambao umekuwa ukitolewa na Mfuko wa Hifadhi wa LAPF kwa wanachama wake.

Akizungumza jana, Meneja Masoko na Mahusiano wa mfuko huo, James Mlowe, alisema utaratibu huo ulianza Novemba, mwaka jana na tayari Sh. Milioni 160 zimekwisha kutumika.

Alisema lengo la kubuni mradi huo ambao wanashirikiana na Benki ya NMB, ni kuwaepusha wanachama wao kutoishi katika makazi holela.

Aidha, alisema mafanikio mengine ambayo mfuko huo umeyapata ni pamoja na kukua kwa thamani kutoka Sh. Trilioni moja mwaka jana hadi Sh. Trilioni 1.87 mwaka huu, huku wakiwa na wanachama 160,000.

Akizungumzia mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 10 hadi 11 jijini Arusha, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama, Venerian Mablangeti, alisema huo ni mkutano wa nane tangu waanze.

Mablangeti alisema kufanyika kwa mikutano hiyo licha ya kutimiza sheria ya uundwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii, umelenga kuwakutanisha wanachama na kuweza kujua taarifa mbalimbali kuhusu michango yao.

No comments: