Hakuwa na muda wa kusubiri, ilipofika majira ya saa moja na
nusu usiku akaanza kujipara na kuvalia viguo vyake vya mawindoni. Akapendeza
sana na ukichangia shepu yake na sura yake nzuri, unaweza kudhani hajazaa kumbe
amepitia mambo magumu sana katika maisha yake tena angali akiwa binti mdogo
sana.
Mwenyewe akikumbuka haya huishia kumwaga machozi, akajifuta
na kujipaka make up kisha juu ya kile kiguo chake akavaa mtandio mwepesi bila
kusahau kubeba kanga ambayo siku zote huwa haiachi ndani ya pochi yake.
Akanyanyua simu yake na kumpigia dereva wake wa bajaji.
Wakati anamsubiria ndipo kisirani wake akaamka; “nakuona hapo changudoa unaenda
kukiuza!” aliropoka Batuli akimtania mwenzake.
“Bora mimi kuliko wewe malaya mkimyakimya unatembea na mizee
kwa ofa za bia! utakufa maskini. Halafu hela ya umeme zamu yako wiki hii,”
alijibu mashambulizi Joy.
Akasikia bajaji inanguruma nje akachungulia na kugundua
ni bajaji akatoka na kwenda kupanda.
“Joy, kwa hiyo hatuli dada angu!” alisema Batuli kwa unyonge
lakini Joy aliondoka kimyakimya kama hajamsikia, akasahau kabisa kuhusu kuchoma
vile vitambulisho na business card ya yule mteja wake wa jana aliyempa bingo ya
laki mbili.
Akashuka windoni kwake akakiachia kimini chake, akatazama
saa yake ya mkononi akagundua ni saa 3 usiku ni muda muafaka kwa ajili ya kazi,
Akanunua kiroba kwenye duka la karibu na kujibust nacho ili kukata aibu.
Akasimama uchochoroni, akapata mteja wa kwanza, kisha wa pili, lakini wakati
anajiandaa kwa ajili ya watatu ghafla akajikuta ameshikwa mkono.
‘Loh ni askari tena wakiwa na defenda, ndani yake wakiwa
wamewajaza wenzake kibao, naye akapakiwa
ndani na safari ya kuelekea Oysterbay kituo cha Polisi ikaanza.
Walipofika kituoni na kuingizwa selo ilikuwa ni kawaida kwa
Joy na wenzake ambapo walimalizia masaa machache ya usiku huo na asubuhi ikawa
safari ya kuelekea mahakama ya jiji pale Posta karibu kabisa na Kanisa katoliki
la St Joseph.
Hapo hutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au jela miezi
mitatu kwa kosa la uzurulaji na hiyo inatokana na ukweli kwamba sheria ya
Tanzania haisemi chochote kuhusu biashara ya ngono hivyo, hata kama polisi
watawakamata machangudoa ni lazima wawashtaki kwa kosa la uzurulaji na si
vingine.
Hizo ndiyo hatua ambazo Joy akiwa na machangu wenzake
walitazamia kuzipitia. Kwa kuwa wengi wao wamezoea kupandishwa mahakamani mara
kwa mara na kutoa faini hiyo ya shilingi elfu hamsini, waliona ni jambo jepesi
kwao na kuhakikisha hakuna changudoa mwenzao ambaye atakwenda jela, machangudoa
kwenye kijiwe cha Joy walikuwa na mfuko wa kusaidiana yaani kama vile vicoba
ambapo kila mmoja huchangia shilingi elfu tano kwa wiki ili iwasaidie kwenye
masuala kama hayo.
Yaani hata kama changu mwenzao amefiwa hao ndiyo humchangia
shughuli nzima za mazishi, sasa vuta picha msiba umedhaminiwa na machangu!
Walikaa ndani ya selo ya mahaka wakiwa na wafungwa wengine
wa kike toka sehemu mbalimbali, wakitarajia kesi yao itasikilizwa mapema saa 2
kamili ili saa 4 waondoke hapo mahakamani, lakini tofauti na walivyotarajia
hadi majira ya saa 6 asubuhi, hakukuwa na dalili yoyote ya kesi yao kusomwa.
Ilipofika saa 8 mchana walisikia afande mmoja wa magereza
akizungumza na wenzake; “Sasa kama hakimu hajaja na hawa machangu si nao
tuwapeleke Keko, wakalale hadi kesho?”
“Nini tunapelekwa jela?” aliropoka Suzy akiangua kilio. Kama
ulikuwa haujui Suzy mmoja wa machangu wakubwa kijiweni kwa akina Joy na alikuwa
mke wa mtu. Hivyo kwa vyovyote hofu aliyokuwa nayo yeye ilimzidi kila mtu hapo
ndani maana kama mumewe akimtafuta na kugundua kumbe aliwekwa ndani kwa kujiuza
itakuwaje!
Je nini kitafuata Usikose Jumatatu
No comments:
Post a Comment