Social Icons

Wednesday 11 May 2016

WANANCHI WATOA MAONI JUU YA MABASI YA MWENDO KASI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
index 
 Na Lorietha Laurence-Maelezo
………………………………………
Baada ya  kuanza rasmi kwa mabasi ya mwendo wa haraka  Jijini Dar es Salaam wananchi wameupokea kwa maoni tofauti  huku wengi wao  wakisifia hatua hiyo  ya serikali katika kurahisisha hali ya usafiri katika jiji hilo.

Wakitoa maoni  yao katika maeneo mbalimbali ya jiji ,Bw.Kulwa Khamis Mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi mwisho amesema kuwa huduma hii ya usafiri ni nzuri kwa kuwa haina foleni na inaokoa muda wa kusafiri.
“nimefurahishwa na huduma hii kwa kuwa haina foleni na inasaidia kufika kwa wakati maeneo yetu ya kazi  na hata kurudi nyumbani mapema,jambo ambalo  linapunguza muda mwingi uliokuwa ukipotea katika foleni” alisema Bw.Khamis.
Naye Bi.Emmy Jonas mkazi wa Kibamba amesema kuwa huduma hiyo ni nzuri lakini amedai kuwa nauli ni kubwa na kuomba uongozi wa Dar es Salaam Rapid Transport (DART)  na taasisi husika kufikiria  upya   nauli ili wananchi wa hali ya chini  waweze kumudu.
Aidha Bi. Jonas ameiomba serikali kumalizia miundombinu ya barabara ya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) ili yaweze kufika mpaka Kibaha, badala ya Kimara mwisho ili kuepukana na usumbufu wa kupanda magari.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mawasiliano  wa BRT, Bw. Abraham Nyatori ameiomba  jamii ibadilike  kuhusu utunzaji wa miundombinu,“hakuna kitu kinaitwa mali ya umma”,amesisitiza Nyatori.
Mtaalam huyo alikuwa na  maana kwamba  kila mwananchi anatakiwa kulinda na kuitunza miundombinu ili itumike kwa muda mrefu na kuiona kama mali yake na siyo ya umma.
Serikali imekuwa ikijenga barabara katika maeneo mbalimbali jijini  na baadhi ya  barabara hizo kuharibika baada ya muda mfupi na  hivyo kuigharimu serikali  mamilioni ya fedha kwa ajili ya matengenezo badala ya kujenga barabara zingine .

No comments: