Social Icons

Tuesday 28 June 2016

WAKULIMA WADOGOWADOGO NA WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA KILIMO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo  juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa wanawasikiliza wenzao wakati walipokuwa wanawasilisha mada walizopewa
Muwezeshaji kutoka Forum CC Feizal Ally Akiongoza majadiliano juu ya uandaaji wa bajeti ya kilomo na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanawathiri kwa kiasi kikubwa wakulima wadogo wadogo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wakulima wadogo wadogo wakichangia mada juu ya changamoto wanazozipata katika kuandaa Bajeti na kutoshirikishwa 
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakichangia juu ya mabadiliko ya Tabianchi yanavyosababisha athali katika kilimo.
 Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Picha na Fredy Njeje

Dar es salaam, Wanawake wakulima wadogowadogo wakiongozwa na waliokuwa  washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na shirika la Oxfam, wamekutana pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na baadhi ya wanafunzi kutoka elimu ya juu, Tanzania kujadili  Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17  na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akifungua Mkutano huo wa siku tatu,  Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka Kibona alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya majadiliano juu ya Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali ilivyo sasa ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia kuibua changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau suala la mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa katika kilimo.

Akizungumza  katika mkutano huo Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema mabadiliko ya Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko ya tabia nchi mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba changamoto kubwa zaidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji chumvi kuingia nchi kavu na kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua kwa kina cha maji katika mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao.

Alisema kuwa  mambo yote hayo yamekuwa yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana na changamoto hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi ya mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto, matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.

Nao wakulima hao kwa nyakati tofautitofauti walizungumzia suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa changamoto nyingi wanazozipata kwa kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na elimu na huduma mbalimbali zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo basi kupitia mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji wa bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya kilimo nchini.





No comments: