Social Icons

Monday 6 June 2016

WOMEN CHARITY GROUP WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MATATIZO YA VICHWA KUJAA MAJI NA MGONGO WAZI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Kwa ufupi Women Charity Group ni  kundi la wanawake na mabinti wanaomtumikia Mungu kupitia maombi, kuombea Familia,Taifa na mambo mengine mengi . Pia hufanya kazi za kujitolea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ocean Road  ambapo walitoa msaada kwa watu wenye Saratani mwaka 2014,  mwaka 2015 walitembelea Mburahati kwa watoto yatima waishio na masista,  mwaka huu wameweza kwenda Muhimbili kutoa msaada kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi.
Wanakikundi cha  Women Charity Group wakiwa wanaingia katika Hospitali ya Muhimbili pamoja na Baadhi ya vitu vyao walivyokwenda kutoa msaada kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na migongo wazi.
  Baadhi ya wanakikundi cha Women charity group wakitoa msaada katika wodi ya watoto hao.
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitoa Shukurani zake baada ya kupokea msaada huo
 Kikundi cha Women Charity wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada huo.

No comments: