Sabasaba
Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya
Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Katikati ni Mkurugenzi
wa Fedha Regina Semakafu na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda
Ngongi. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya
kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
***********
NUSU
ya kwanza ya Mwaka 2016 iliyoisha mwezi Juni, imekuwa yenye mafanikio
makubwa sana kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Pamoja na changamoto
mbalimbali ambazo bado zinaikabili benki yetu, kwa kipindi kirefu sasa,
lakini Benki imefanikiwa kupata faida kabla ya kodi ya shilling bilioni
8.84 ukilinganisha shillingi bilioni 5.48 zilizopatikana kipindi kama
hicho mwaka 2015,ambayo ni sawasawa na ukuaji wa asilimia 61.47%.
Ukuaji
huu wa faida katika kipindi hiki cha nusu mwaka wa 2016 umewezesha
kukua kwa mtaji wa wawekezaji hadi kufikia shillingi billioni 48 kutoka
shillingi bilioni 37 mwezi Juni mwaka 2015.
Mapato
ya Benki kwa nusu mwaka 2016 yaliongezeka hadi kufikia shilling bilioni
42.5 kutoka bilion 34 iliyofikiwa nusu ya mwaka 2015, huu ni ukuaji wa
asilimia 38%. Vilevile katika kipindi hichohicho amana za wateja
ziliongezeka na kufikia shilingi bilioni 294.64 kutoka shilingi bilioni
263.68 June mwaka 2015, ukuaji wa asilimia 11.74%.
Mikopo
imeongezeka hadi kufikia shillingi billioni 278 kutoka shilingi
billioni 241.51 Juni mwaka 2015, ongezeko la asilimia 15.22%. Sehemu
kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na
wafanyakazi wa sekta ya umma na serikali kuu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Rasilimali
za benki zilikuwa hadi kufikia shilling 390.8 bilioni mwezi Juni mwaka
huu 2016 kutoka shillingi billioni 333.96 Juni mwaka 2015 ongezeko la
asilimia 17.16%.Benki ya Posta kwa mwaka 2016, iliendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, ambapo Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Msajili wa Hazina Bw.Lawrence Mafuru.
Matawi
hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Benki
ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa
Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama.
Pia,
benki imehamisha tawi lake la Moshi kwenda kwenye jengo jipya la NSSF,
na hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda
kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za
kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya
kisasa zaidi.
Hadi
hivi sasa TPB inayo matawi 30 na madogo (min branches) 30, Mashine za
kutolea pesa (ATM) zinazo milikiwa na benki ya posta ni 38 na 200 za
umoja wamabenki (Umoja switch), hivyo kuwawezesha wateja wetu kupata
huduma ya pesa nchi nzima.
Pia benki inao mawakala wa benki 133 kupitia TPC,na vituo vya huduma 200 kupitia mawakala binafsi.
Benki ya posta inaendelea na jitihada zake za kuongeza wigo wa biashara kwa njia mbalimbali, zikiwemo:
kutoa
mikopo kwa vikundi vidogo vidogo (group lending), ambapo hadi sasa
tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 6.5 bilioni na huduma ya
kuwakopesha wazee (wastaafu loan) kupitia mifuko ya jamii kama vile
PSPF,NSSF na ZFF, ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi
56 bilioni.
Kwa
kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
enki imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 541 ili kuviinua
kiuchumi vikundi vilivyo chini ya Baraza hilo.
Kufungua account za vikundi visivyo rasmi(VICOBA informal groups) ambapo hadi sasa akaunti 30 elfu zimefunguliwa.
Huduma
za kibenki kupitia simu za kiganjani,ambapo kwa kipindi cha nusu ya
mwaka huu akaunti 271,427 zilifunguliwa, kulinganisha na akaunti 236,981
zilizofunguliwa hadi mwishoni mwa mwaka jana. Hili ni ongezeko la
akaunti 34,446, sawasawa na asilimia 15.
Benki
ya Posta imejidhatiti kuendelea kutoa huduma bora, nafuu na za kisasa
kwa maana ya kutumia teknolojia zaidi katika kipindi hiki. Tunaamini
kwamba bado kwa kutumia teknolojia ya TPB POPOTE tutaweza kuwafikia
Watanzania walio wengi hasa vijijini ambao bado hawajaingia kwenye mfumo
wa kifedha.
Pia
benki itaendeleza na kuboresha mahusiano yake na makampuni za simu ili
kuweza kupeleka huduma zake karibu zaidi na wananchi, na pia ushirikano
wake na Saccos pamoja na Vicoba.
Benki
ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla
kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi
hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama
nafuu.
Pia
shukrani za pekee ziende kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa uongozi wao
thabiti na usimamizi imara, unaoendelea kuhakikisha kuwa benki inakuwa
miongoni mwa taasisi bora za kifedha hapa nchini.
No comments:
Post a Comment