Social Icons

Monday, 1 August 2016

HOT: WALIMU WAKAMATWA KUTEMBEA NA WANAFUNZI, WAWILI WAHAHA, MWANAFUNZI MMOJA KIDATO CHA KWANZA ATIWA MIMBA ,KILIMANJARO

 Mmoja wa wanafunzi hao ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa akiwa anasomewa ujumbe na mwalimu mmoja wapo namna walivyokuwa wakichati na mwalimu jumbe za mapenzi

 Mmoja wa walimu akiwa anamsomea mzazi mambo ambayo mwanae alikuwa akiwasiliana na moja ya walimu wa shule hiyo
 Hizi ni Baadhi ya karatasi ambazo waliandika walimu wanaotembea na wanafunzi na kubainika mwalimu mmoja anatembea na zaidi ya mwanafunzi mmoja
Diwani wa kata hiyo ambayo haikufahamika mara moja Bw. Pantaleo Lyakurwa aliyekaa akiwa anasikiliza mashitaka hayo

Na mwandishi wetu Blogs za Mikoa
Walimu wanne ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sasa wamekamatwa wakiwa na mahusiano ya kimapenzi na Mabinti wa shule mojawapo ya Sekondari iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ambayo pia jina lake limehifadhiwa.

Walimu hao wamebainika baada ya kufanyika msako mkali wa kukamata wanafunzi wanaotumia simu za kiganjani kinyume na utaratibu wa shule hiyo, ambapo walikagua ujumbe mfupi wa maneno yaani SMS kwenye simu hizo ndipo walipokuta walimu hao wakiwasiliana na wanafunzi hao kwa meseji zilizoashiria mapenzi.

Baada ya kupata taarifa hizo Diwani wa eneo hilo Bw. Pantaleo Lyakurwa alifika na Askari wa Jeshi la Polisi  katika shule hiyo na kuwakamata walimu wawili ambapo wamefikishwa Polisi na walimu wengine wawili bado wanasakwa.

Bwana Lyakurwa amewaonya vikali walimu ambao wanaendelea na tabia za kutembea na wanafunzi na kutoa agizo kuwa atakayebainika atakamatwa na kufikishwa Polisi, Mahakamani kisha kusimamishwa kazi.

Wakati huo huo kuna Binti wa miaka 15 kidato cha kwanza  ambaye pia alikamatwa akitembea na mmoja wa walimu hao aliwaacha watu mdomo wazi baada ya kugundulika kuwa ni mjamzito lakini cha ajabu aligoma kumtaja mtu aliyempa ujauzito huo.

No comments: