Social Icons

Wednesday, 3 August 2016

TUKIO RASMI KATIKA PICHA : TV1 KURUSHA LIVE LIGI KUU YA UINGEREZA 'PREMIERE LEAGUE' BURE #TorokaujeTV1

 Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Say akitoa utangulizi wa programu hiyo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)
 Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu akitoa ufafanuzi wa programu hiyo.
Mkuu wa Uzalishaji Vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo akielezea jinsi kipindi hicho kitakavyorushwa. 
 Meneja  Masoko wa Startimes, Damien Li akielezea ushirikiano wao na TV1 katika kuhakikisha Ligi hiyo inaoneshwa laivu na bure.
  Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah akizungumzia uwepo wake katika uchambuzi wa  Ligi Kuu ya Uingereza itakayorushwa na live na TV1
 Mwendeshaji wa vipindi vya Ligi Kuu ya Uingereza kutoka TV1, Ally Kashushu akiwaahidi makubwa watazamaji na mashabiki wa soka.
 Blogger Mkongwe hapa Nchini anaye endesha Libeneke la Kajunason Cathbert Kajuna akiuliza swali wakati wa Mkutano huo wa TV1 na waandishi wa habari 
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo
 Hapa waandishi wa habari wakiwa katika studio zitakazotumika kwa ajili ya kurekodia uchambuzi wa Ligi hiyo.
 Mkuu wa Uzalishaji Vipindi, Mukhsin Mambo akiwaelezea jambo waandishi wa habari waliofanya ziara ya studio hizo.
 Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah akiwa katika eneo ambalo watakuwa wakifanyia uchambuzi wa Ligi hiyo
 Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah(Kulia) akiwa na Mwendeshaji wa vipindi vya Ligi Kuu ya Uingereza kutoka TV1, Ally Kashushu sehemu watakayokuwa wakifanyia uchambuzi huo

Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa 
Na Chande Abdallah Dar es salaam yetu Blog

Kituo cha Televisheni nchini, TV1 leo hii kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.

Akizungumzia kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1,  Joseph Sayi alisema kuwa Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha Startimes, Watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure bila gharama yoyote.


Naye Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi, pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali, matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.


Akizungumzia kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo, alisema kuwa  kipindi hicho kitakachoanza kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na Ally Kashushu.


Aidha Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.

Imeandaliwa na Blogs za Mikoa Tanzania kupitia www.blogszamikoa.com , blogzamikoa@live.com 0653146563


 

No comments: