Social Icons

Monday 31 October 2016

Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejephotography Twitter @Fredynjeje
Winner “Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.” Alisema Olive huku akitoka machozi baada ya kutangazwa mshindi. 880A9842 Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.
Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio waliofanikiwa kuingia fainali. 880A0015 880A0011 880A0009 880A0005 Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa jana usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two.Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce Sambuta, Alex Essau, Olive Kiarie, Irene Ishengoma na Ngenda Pilly.[/caption] Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya mshiriki mdogo wa kike. Top 3 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishengoma Top 3 ya Maisha Plus Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishongoma[/caption] Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo. 880A9978 880A0043 880A0055   880A0125 880A0127 880A0129 880A0130 880A0132 880A0134 880A0166 880A0169 880A0172 880A0184 880A0210  

No comments: