Social Icons

Sunday, 2 October 2016

TUKIO RASMI KATIKA PICHA: ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi waHarambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa
 Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza
Baadhi ya waumini wakifatilia neno la Mungu
 Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno
Baadhi ya waumini wakiendelea kuchukua mambo muhimu wakati somo linaendelea 
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno
 Waumini wakifuatilia neno kwa Makini
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini
 Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini
 Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa
 Wakijiandaa Kumtukuza Mungu
 Mitambo inakaa sawa
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele wakati akisisitiza jambo
 Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabeleakiimba nyimbo za Sifa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo 
 Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu  kwa njia ya Nyimbo za Sifa
 Waumini wakiimba nyimbo za Sifa
 Nyimbo za Sifa zikiendelea
 Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali(Kulia) akiwa na Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond
 Wakiendelea kusifu na Kuabudu
Picha zote na Fredy Njeje 
Instagram: @fredynjejephotographyKanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi hii leo.

Akizungumza katika misa iliyofanyika mapema leo mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa leo kanisani hapo kwa waumini na watu mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu. 

Mbali na hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia  ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote  ambapo pia alisema kuwa zoezi la harambee  litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.

“Sisi kanisa letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha, aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huohuyo.

No comments: