Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez amesema vijana ndio chachu kubwa ya
maendeleo endelevu kama watatumika ipasavyo.
Alisema
kwa nchi kama ya Tanzania, yenye idadi yake ya vijana ipatayo milioni
30 ni vyema ikajielekeza katika namna ya kuiitumia vyema nguvu hiyo.
Akizungumza
katika mafunzo ya kuwezesha vijana kutambua malengo ya maendeleo
endelevu (SDGs), alisema ni vyema watu wakatambua umuhimu wa kuungana
pamoja kukabiliana changamoto zilizopo.
Alvaro
ambaye alikuwa akitoa mafunzo kwa vijana na kujibu baadhi ya maswali
yao mwishoni mwa wiki alisema kwamba maendeleo yanahitaji kufanyiwa kazi
na kwamba kuwapo kwa mifumo ya kupasha habari ya kisasa sio sababu ya
kuwezesha au kukwamisha maendeleo.
Alisema
mifumo ya kupashana habari ya kisasa kama mitandao ya kijamii ambayo
inaonekana kama ndio njia pekee ya kufikia taarifa haikuwapo wakati
mataifa ya magharibi yanaendelea, hivyo suala la mifumo hiyo si kitu cha
ziada zaidi ya juhudi binafsi ya kukabiliana umaskini kabla ya kujiunga
kwa pamoja .
Alisema
nadharia ya uwingi ndio ya msingi katika utekelezaji wa malengo
endelevu kwa kuwa inatafsiri malengo hayo katika utekelezaji kuanzia
ngazi za serikali na mipango yake.
Alisema
vita ya sasa ya kukabiliana na umaskini wa uliokithiri inaweza
isifanikiwe lakini kuondoa umaskini wa aina hiyo inawezekana kama ilivyo
katika mataifa ya China, India, Korea na hata Chile.
Maendeleo
endelevu yenye malengo 17 yamedhamiria katika miaka 15 ijayo kuleta
uwiano wa maendeleo katika nchi moja moja na kwa ujumla ili kukabiliana
na mabadiliko ya tabia nchi na umaskini ambayo ndio malengo ya haraka.
Maendeleo
endelevu (SDGs) yamejipanga kutekelezwa kuanzia yaliposhia malengo ya
milenia ikiwa ni msukumo mpya wa kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii
duniani kote.
Kwa
mujibu wa Alvaro malengo hayo ambayo yamejikita zaidi kukabili umaskini
uliokithiri lakini pia kuleta mizania katika maeneo matatu ya maendeleo
endelevu kwenye uchumi, jamii na mazingira amewataka vijana hao
kuhakikisha kwamba wanajitolea kwa kuwa misaada haijawahi kuamsha
maendeleo.
Alisema
ruzuku na misaada si kichocheo cha maendeleo na kwamba maendeleo
yanaweza kuangaliwa kwa kuangalia pia dhima ya kisiasa, kidini au
nyinginezo ambayo inatoa majibu ya namna ya kuenenda katika kukamata
ustawi wa jamii.
Alisisitiza
katika maelezo yake kwamba serikali nyingi zimekuwa zikikabiliana na
rushwa kwa lengo la kukabiliana na umaskini uliokithiri huku akiipongeza
serikali ya Tanzania kuona kwamba vita yake kubwa ni kukabili umaskini
lakini pia kwa kukabili rushwa.
Alisema
kuishi pamoja na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kutasaidia
kuleta maisha yanayotakiwa ya hali ya juu yenye kujali mazingira
ambatana.
Pia
Alvaro alikumbusha maelezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba
hata mataifa hohehahe yanaweza kubadilisha maisha ya watu wake na
kitaifa kama ilivyofanya China, India na Chile na kwamba mataifa hayo
ambayo miaka 50 iliyopita zilikuwa sawa na Tanzania sasa zina mabadiliko
makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.
Alisema
ni wajibu wa dunia kukabili umaskini uliokithiri kwa kumshirikisha kila
mtu katika malengo hayo 17 bila kumwacha mtu nyuma.
Akijibu
maswali mbalimbali ya vijana kuhusu hatima yao alisema kwamba vijana ni
nguvu kubwa kama itaamua kuwa chanya itawezesha maendeleo na kama
ikiamua kuwa hasi itasababisha mitafaruku mikubwa huku akitolea mfano
kuwa hata Al Shabab walipoamua kukabili serikali kuleta maendeleo
walikubaliana katika mazingira hasi na kuleta vurugu kubwa.
Alisema
Shabab maana yake ni vijana lakini hatua waliyochukua kukabiliana na
umaskini haikubaliki kwa kuwa imekuwa ikichochea ghasia.
lisema
majadiliano yanayoshirikisha vijana ili kuongeza uelewa katika malengo
ya SDGs yatakuwa ni heri kubwa kama yatazingatiwa kwani yatawezesha kwa
namna moja kuona mbele na kushirikiana katika utekelezaji.
Alisema
ni vyema kama utawala bora ulivyoingizwa kwa lengo la kuwezesha
utekelezaji wa malengo mengine kama mazingira na maendeleo ya kijamii
katika elimu bila ubaguzi.
Alisema
kwa sasa suala si kutambua bali namna ya kushirikisha malengo hayo na
mipango ya maendeleo ili kufanya malengo kuonwa kwa wazi na kutafsiriwa
katika maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment