Social Icons

Monday 13 February 2017

MAKONDA AKABIDHI MAJINA MENGINE 97 KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA SIANGA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejephotography Twitter @Fredynjeje

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda,  akionyesha majina mengine 97 ya wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya awamu ya tatu wakati akimkabidhi majina hayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga, kwa ajili ya kuyafanyia kazi. Makonda alikabidhi majina hayo leo mchana wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa majina ya awamu hii ya tatu yatatikisa nchi kwani wameanzia toka uongozi wa awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu,Benjamini Mkapa, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. 
CHANZO MAFOTO BLOG


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, 
Rogers William Sianga 
ili yaanze kushughulikiwa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo amekabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William sianga kuwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa.

Shekh wa Mkoa wa Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Alhadi Mussa akizungumza na watendaji mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi, Wenyeviti wa serikali za mitaa na madiwani pamoja na vijana mbalimbali waliokuwa wanatumia dawa za kulevya katika mkutano wa taarifa ya maendeleo ya Kampeni ya kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed, TID, akizungumza na kutoa ushuhuda, na kuahidi kutoa ushirikiano katika Vita ya kupambana na madawa ya kulevya.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Mchungaji Geoge Fupe akizungumza katika mkutano huo wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza jambo na Bw. Rogers William sianga kuwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya katika mkutano wa kutoa tathmini ya kampeni ya kutokomeza madawa ya kulevya Kamishna katika mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika mkutano huo.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Saimon Sirro akizungumzo wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo leo.

No comments: