Bi. Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha Ushawishi na utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania, Akifungua mkutano na kuelezea madhumini
yake kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Bw.Francis Odokorachi.
Mratibu
wa NES Bw. Benard akielezea namna wanavyofanya kazi na wadau wengine
katika maswala ya ardhi, ambapo alielezea kwa undani namna ya kuangalia
haki za wanawake katika umiliki wa Ardhi,pamoja na hayo aliongeza kuwa
wanafanya kazi pamoja na mashirika 14 wakiwemo Oxfam na TARA. Mwisho
alieleza kipaumbele chao ni kampeni katika mambo yanayohusiana na Ardhi.
Profesa
Majourin Mbilinyi Mwanamke Mwanaharakati,akielezea kuhusu jinsia na
ukombozi kwa wanawake, alisema mwanake hawezi kukomboka bila kuwa
mkombozi wa jamii, alisema kuwa ni muhimu sana kuwakomboa wanawake
wadogo wadogo ambao wanazalisha chakula ili wawe na haki ya umiliki wa
Ardhi .
Baadhi
ya wajumbe wakiendelea kufuatilia na kuchukua mambo mbalimbali muhimu
katika mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili namna
watakavyofanya kampeni ya haki ya wanawake katika kumiliki Ardhi.
Bi. Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha Ushawishi na utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania, akizungumzia umuhimu wa wanawake katika
kumiliki ardhi kwa sababu mwanamke anashiriki kwa asilimia kubwa katika
kuzalisha Chakula na kutengeneza bidhaa mbalimbali katika kujipatia
kipato, alisema kuwa ni muhimu kwa wanawake kuwa na haki sawa katika
umiliki wa ardhi na pia mashirika ya kimataifa kushirikiana na wazawa
katika kuhakikisha mambo yanayohusiana na ardhi yanaenda vizuri.
Mratibu
wa Miradi ya Ardhi kutoka Care International Bi. Mary Ndaro akielezea
kuhusu idadi kubwa wanawake wanaozalisha mazao ya chakula wanaishi
vijijini na wanategemea Ardhi katika swala zima la maendeleo na
kujipatia kipato katika kuendesha maisha yao, aliongeza kuwa ili kampeni
hii iendelee wanawake wanahitaji msaada wa karibu.
Mratibu
wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bi.
Naomi Shadrack akizungumza namna akielezea namna wanavyofanya kazi
kuhusiana na maswala ya ardhi na ushiriki wao katika kampeni ya wanawake
katika kumiliki ardhi
Bi.
Josephine Dungumaro(Kulia) Mshauri wa Jinsia kutoka Shirika la
kimataifa la utafiti wa Mifugo akielezea namna shirika lao linavyofanya
kazi na kugusia maeneo wanayofanyia kazi ni pamoja na Kiteto,Chalinze na
Bagamoyo.
Bi. Amina Ndiko(Kulia) kutoka Oxfam akisisitiza jambo kuhusu maswala ya wanawake na umiliki wa Ardhi.
Mwezeshaji Bw. Evans Rubara akiendelea kutoa Mwongozo
Bi Nuria Mshare akiwasilisha Mada iliyohusu 'Harmonization of Land Laws'
Mshiriki
wa Shindano la Mama Shujaa Msimu wa nne Bi. Edna Kiogwe akiwasilisha
mada juu ya 'Elimu ya wanawake kujua haki zao za ardhi'
Bi.
Wigayi Kisandu Mwanasheria kutoka WLAC, amezungumza namna ya wanawake
wanavyopewa nafasi ndogo katika kumiliki ardhi na kufanya juhudi za
kuhakikisha wanapata nafasi ya kumiliki ardhi.
Mkutano ukiendelea
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania.
No comments:
Post a Comment