Social Icons

Wednesday 13 September 2017

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI(NLUPC) YAENDESHA MKUTANO WA WADAU JUU YA USIMAMIZI WA MATUMIZI YA ARDHI,UHIFADHI WA MAZINGIRA NA BIOANUAI KATIKA UKANDA WA UDZUNGWA,MAGOMBELA NA SELOUS.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra, akifungua  warsha  hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi hiyo Dkt. Stephen Nindi

Wadau mbalimbali wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra wakati akitoa maneno ya utangulizi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa  ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akiwasilisha mada juu ya  Sera,Sheria, Miongozo na Uratibu katika upangaji,utekelezaji na usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Bi Tabu Njonde akiuliza swali na kutaka kujua migogoro kati ya kijiji na kijiji ina adhari gani na namna gani wanaweza kuepukana nayo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katurukila Bw. Salumu Lubala akiuliza swali juu ya Umilikishwaji wa Ardhi.
Afisa Mipango Miji kutoka wilaya ya Kilombero Bw. Remigi Lipiki akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa warsha hiyo.
Afisa Ardhi Mteule kutoka Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa warsha hiyo.
Afisa Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife Foundation ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika ukanda wa Udzungwa,Magombera na Selous,utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
Wadau mbalimbali wakimsikiliza Bw. Mwakipesile akiwasilisha mada
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkula Bw. Christopher Kafunga akitaka kupata ufafanuzi  kuhusu kupata mkopo wa fedha kutoka Benki kwa kutumia hati miliki ya ardhi.
Diwani wa Kata ya Msolwa Station Mh. Hakim Songa akiuliza maswali kuhusiana na maswala ya ardhi na umilikishwaji
Afisa uhifadhi na usimamizi wa Mazingira na usafi kutoka Wilaya ya Kilombero Bw. Samwel Mtafya akijibu maswali mbalimbali yaliyohusu mazingira.
Msaidizi wa Misitu Mwandamizi kutoka Wilaya ya Kilombero Bw. Peter Nkunga akijibu maswali mbalimbali yaliyohusu maswala ya maliasili.
Bi Maria Sengelela Afisa Miradi wa asasi ya kiraia ya Solidardad akielezea jinsi wanavyoshirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika kuhimiza matumizi Bora ya Ardhi
Bw. Eugine Cyrilo kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akichangia jambo kuhusiana na maswala ya mazingira
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akitoa neon la kufunga warsha hiyo.
 Diwani wa Kata ya Mang'ula Mh. John Mjami akitoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa warsha hiyo na kusema kuwa imewasaidia kupata majibu ya kwenda kuwapatia wananchi wao na kuendelea kuwapa elimu zaidi juu ya usimamizi wa matumizi ya Ardhi,uhifadhi wa Mazingira na Bioanuai.
Wajumbe wakiendelea kufuatilia warsha hiyo iliyofanyika Mang'ula Kilombero
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya ardhi (NLUPC) imewasilisha Taarifa ya tathimini na kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya umiliki wa Ardhi,mipango ya matumizi ya ardhi na hifadhi ya mazingira, utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na African Wildlife Foundation.

Akizungumza na wadau wa mpango wa matumizi ya Ardhi kutoka kata za Mkula, Mang’ula, Msolwa Stesheni pamoja na Sanje Bi. Albina Burra  alieleza kuwa  Tume hiyo inamalengo ambayo ni kuhakikisha kuwa kunatayarishwa na kunatekelezwa mipango shirikishi ya matumizi ya ardhi kwa minajili ya usawa wa usalama wa miliki za Ardhi, kuongeza uzalishaji wa Ardhi, uhifadhi wa mazingira na Bioanuai.

Alisema kuwa Kilombero ni wilaya Muhimu sana katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ipo katika ukanda wa mradi mkubwa wa Taifa wa kuimarisha kilimo wa SAGCOT pia ina wingi wa lasirimali nyingi za Ardhi na mazingira zikiwemo za wanyamapori,ardhi yenye rotuba,misitu,vyanzo vya maji,Bonde kubwa la Afrika ambalo lina mito mitatu ambayo ni Ruaha,Rufiji na Ruevu, Milima ya Udzungwa, Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa Reserve.

“Utafiti fiti huu ulifanywa na wataalamu kutoka tume wakishirikiana na watu wa African Wildlife Foundation na walihusisha kanda mbili kwanza kuna Udzungwa,Magombela na Selous kanda ya pili ni Korido ya Mgeta” Alisema Burra. Na kwamba wamewashirikisha wadau hao kwa kuwa na wao wanafanya tafiti zinazofanana ili kuwepo na uhusishwaji wa sekta hizi kwa ajili ya uboreshaji wa kufanya kazi bila kuleta Migongano na athari za kimazingira.

Aliongeza kuwa warsha hiyo ni muhimu kwa kuwa wajumbe walipata tathmini juu ya umilikishwaji wa ardhi na kuona kama vijiji vyote vinamipango ya matumizi bora ya ardhi na pia kuona kama vijiji vina vina hati za Kijiji na wakazi wangapi wana hati za Kimila.

Mwisho alizungumzia kuhusu Sera,Sheria, Miongozo na Uratibu katika upangaji,utekelezaji na usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

Warsha hiyo ilihusisha ukanda wa Magombera-Udzungwa-Selous ,kulikuwa na kata nne ambazo ni Msolwa Stesheni,Nkula, Mang'ula B na sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni,Nkula,Sonjo,Msufini,Katurukila,Kanjenja, Magombera na Sanje. 

Washiriki katika warsha hiyo walikuwa ni Madiwani, ma Afisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Maafisa watendaji wa Vijiji,Wenyeviti wa Vijiji, na wajumbe wa Serikali za Vijiji.



No comments: