Social Icons

Friday 15 September 2017

WADAU WA KORIDO YA MNGETA WAPOKEA TATHIMINI YA UTAFITI WA USIMAMIZI WA MATUMIZI YA ARDHI,UHIFADHI WA MAZINGIRA NA BIOANUAI KUTOKA TUME YA TAIFA YA MIPANGO NA MATUMIZI YA ARDHI(NLUPC)

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra, akifungua  warsha  hiyo na wadau katika Korido ya Mngeta kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi hiyo Dkt. Stephen Nindi na
mada juu ya  Sera,Sheria, Miongozo na Uratibu katika upangaji,utekelezaji na usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife Foundation ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika ukanda wa Mngeta juu ya,utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
Mjumbe wa kata ya Mchombe Kijiji cha Njage Bw. Jepemi  Kankoselo akiuliza swali juu ya nini kifanyike ili kurudisha njia walizokuwa wanapita wanyama wa zamani ambazo zimezibwa kutokana na wananchi kuweka makazi maeneo hayo.
Diwani wa Kata ya Mawala Mh. Godfrey Lwena akiuliza maswali mbalimbali yanayohusiana na maswala ya ardhi katika eneo lake
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbingu Bw. Samora Mbuna akiuliza swali la ni namna gani ya kupata hati Miliki na kutaka kufahamu
Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Bi. Devotha Salukele akijibu Maswala mbali mbali yahusuyo sheria yaliyoulizwa na wananchi kuhusu Ardhi.
Bi Maria Sengelela Afisa Miradi wa asasi ya kiraia ya Solidardad akielezea jinsi wanavyoshirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika kuhimiza matumizi Bora ya Ardhi

Muwezeshaji  Bw. Geofrey Siima kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akiendelea kutoa utaratibu wa warsha hiyo iliyofanyika Mbingu.
Afisa Maendeleo ya jamii kutoka Asasi ya Kiraia ya African Wildlife Foundation Bw. Fadhili Njilima akielezea namna asasi hiyo inavyofanya kazi na ushirikiano wao na Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akitoa neno la shukurani na kufunga rasmi warsha hiyo

 Diwani wa Kata ya Mchombe Mh.Johan Mwambeso akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wajumbe wote waliofika katika warsha hiyo.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia warsha hiyo
Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania 


Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi  ya ardhi (NLUPC) imewasilisha Taarifa ya tathimini na kupokea maoni kutoka kwa wadau wa Korido ya Mngeta juu ya umiliki wa Ardhi,mipango ya matumizi ya ardhi na hifadhi ya mazingira, utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na African Wildlife Foundation. 

Akizungumza na wadau wa mpango wa matumizi ya Ardhi katika ukanda wa Mngeta Bi. Albina Burra  alieleza kuwa  Tume hiyo inamalengo ambayo ni kuhakikisha kuwa kunatayarishwa na kunatekelezwa mipango shirikishi ya matumizi ya ardhi kwa minajili ya usawa wa usalama wa miliki za Ardhi, kuongeza uzalishaji wa Ardhi, uhifadhi wa mazingira na Bioanuai.

“Utafiti  huu ulifanywa na wataalamu kutoka tume wakishirikiana na watu wa African Wildlife Foundation na walihusisha kanda mbili kwanza  Udzungwa,Magombela na Selous kanda ya pili ni Korido ya Mngeta” Alisema Burra.

Alisema kuwa Kilombero ni Wilaya Muhimu  katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ipo katika ukanda wa mradi mkubwa wa Taifa wa kuimarisha kilimo wa SAGCOT na ina wingi wa lasirimali nyingi za Ardhi na mazingira zikiwemo za wanyamapori,ardhi yenye rotuba,misitu,vyanzo vya maji,Bonde kubwa la Afrika ambalo lina mito mitatu ambayo ni Ruaha,Rufiji na Ruevu, Milima ya Udzungwa na Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa

Alimalizia kwa kusema  kuwa warsha hiyo ni muhimu kwa kuwa wajumbe walipata tathmini juu ya umilikishwaji wa ardhi na kuona kama vijiji vyote vinamipango ya matumizi bora ya ardhi na pia kuona kama vijiji vina vina hati za Kijiji na wakazi wangapi wana hati za Kimila. 

Washiriki katika warsha hiyo walikuwa ni Madiwani, ma Afisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Maafisa watendaji wa Vijiji,Wenyeviti wa Vijiji, na wajumbe wa Serikali za Vijiji. 

Mkutano huo ulihusiha Korido ya Mngeta ambapo kulikuwa  na Kata za Namawala,Igima,Mbingu,Mngeta,Mchombe,Chita na Mofu pia kulikuwa na vijiji 13 ambavyo ni Mofu,Ihenga,Kisegese,Vigaeni,Makutano,Igima,Mbingu,Njage, Mngeta,Mchombe,Lukolongo na Ikule.  



No comments: