Social Icons

Tuesday 24 October 2017

NMB YATENGA BILIONI 1 KWA AJILI YA KUCHANGIA MAENDELEO YA WANANCHI.

    Na  Walter  Mguluchuma.
          Katavi .
  Benki ya  NMB  imetenga  zaidi  ya  Shilingi Bilioni  Moja kwa  ajili ya  kuchangia  maendeleo  ya Wananchi  ikiwemo  kusaidia  sekta  ya   afya  na  Elimu  kiasi hicho  kinaifanya  kuwa  Benki ya  kwanza hapa   katika  kuchangia   maendeleo kuliko Benki yoyote  hapa  Nchini .
  Hayo yalisemwa  hapo jana na   Meneja  Mahusiano   Biashara  ya  Serikali wa  Benki ya  NMB wa Kanda ya  nyanda za juu  Focus   Lubende wakati wa  hafla ya kukabidhi  bati 300 kwa ajiri ya  Shule ya  Msingi Kilida  Katika  Halmashauri ya   Mpimbwe na  Kompyuta  7 kwa  ajiri ya Shule za  Sondari tatu za  Halmashauri hiyo   hafla hiyo ilifanyika  katika  viwanja vya ofisi ya  Halmashauri ya Mpimbwe.

 Alisema kwa  mwaka huu wa 2017 NMB imetenga   zaidi ya shilingi  Bilioni moja  kwa  ajili ya kuchangia  maendeleo  ya  wananchi ikiwemo  kusaidia   sekta ya  afya  na  elimu  na kuifanya  benki  hiyo kuwa  kuwa   benki ya kwanza  katika kuchangia maendeleo  kuliko  benki yoyote hapa  nchini .
  Focus  alieleza kuwa   NMB    ndio  inayoongoza   nchini  kwa kuwa na matawi  mengi  kwani inajumla  ya  matawi 217 na  ATM  zaidi ya 800 kwa  nchi nzima  pamoja na wateja  zaidi ya milioni mbili   ambayo ni hazina  ambayo hakuna  benki  nyingine   yenye  inayo .
 Alisema kwa   miaka   kadhaa  sasa    Benki  hiyo  katika  mipango  yake   imekuwa   ikishiriki   shughuli  mbalimbali  za  jamii  kama  kusaidia  sekta ya elimu  madawati  na viti  kwa upande wa afya wamekuwa wakisaidia   vitanda magodoro na   shuka .
 Pia  huwafariji  jamii  katika  vipindi  vya majanga  mbalimbali  zinazogusa  maisha  ya watu wengi   baada ya kutambua  kuwa  kupitia  jamii   ndipo  wateja wengi  wanapo toka   kwa   hiyo  kurudisha   sehemu  ya faida  kwa jamii ni  utaratibu  wao .
Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi   Meja  Generali   mstaafu  Raphael  Muhuga  aliiomba   benki  hiyo kufungua  matawi  kwenye  maeneo ya   Kata za  Majimoto  na  Usevya  Wilayani  Mlele  na  Kasekese   Wilayani  Tanganyika    kwani  maeneo  hayo yanamzunguko  mkubwa  sana wa  fedha .
Alisema  MNB  ndio   benki   pekee  inayotowa  huduma za  Kibenki  katika  Wilaya ya  Mlele  na imekuwa ikitowa misaada mbalimbali kwenye   jamii katika  maeneo ya  Mkoa wa  Katavi kira mara wanapokuwa wameombwa kufanya hivyo .
Nae  Mkuu wa  Wilaya ya  Mlele  Rachel  Kasanda  alisema  msaada wa  bati  uliotolewa na  benki hiyo   utasaidia  sana  kwenye  shule  ya msingi  Kilida  iliyopata  janga  mwezi machi  mwaka huu  ya kuenzuliwa  paa  lake  na   hivyo kuwafanya wanafunzi  kujifunza katika mazingira magumu.
 Alisema  Kompyuta  saba walikabidhiwa  wamepanga kuzigawa  katika  Shule  tatu za  Sekondai zilizopo  katika  Halmashauri  hiyo ya  Mpimbwe  ambazo alizita kuwa ni  Sekondari ya  Mpinde ,Mamba  na  Usevya.
Katika  tukio  hilo la     janga la  mvua  watu watu  sita walifariki  dunia   baada ya kusombwa na maji  na pia  kulitokea  uharibifu  mkubwa wa   nyumba za  makazi ya watu na barabara.

No comments: