Tume
ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ipo mbioni kuanzisha Kanzidata
(Database) ya mipango ya matumizi ya ardhi iliyofanyika nchini na wadau
mbalimbali wa sekta ya ardhi.
Kwa
kushirikiana na wadau wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya
matumizi ya ardhi wa taasisi za serikali pamoja na asasi za kiraia, Kanzidata
hiyo itabeba taarifa zitakazoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli
mbalimbali kama vile kilimo, malisho, huduma za jamiii, n.k itarahisisha
utendaji kazi kwa Tume, mamlaka zingine za upangaji, wadau pamoja na wananchi
kwa ujumla ambao watatumia teknolojia kujua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya
shughuli mbalimbali nchi nzima
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt.
Stephen Nindi akifungua mkutano wa kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa
uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi
Mwenyekiti wa Kikao Bw. Jamboi Baramayegu kutoka ujamaa Community akielezea utaratibu wa namna kazi itakavyofanyika
Afisa
Tehama kutoka wakala wa Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga akitoa
maelezo ya malengo ya wao kushiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa
uanzishwaji wa kanzi data ya mipango na matumizi ya ardhi.
Afisa
Mipango wa Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Gelard
Mwakipesile, akielezea kwa kina kwa wajumbe wa mkutano kuhusu mipango ya
matumizi ya ardhi,mchakato ulipo anzia hadi kuanza kwa mchakato wa
uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya ardhi
Bw.
Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akichangia jambo wakati wa kikao
cha mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya matumizi ya
ardhi.
Baadhi
ya wanakikosi kazi kutoka sekta mbalimbali wakiendelea na majadiliano
ya kutoa maoni yao juu ya kuandaa mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data
ya mipango ya matumizi ya ardhi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye akiwasilisha
mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya
mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la wafugaji
Bw.
Godfrey Massay Meneja utetezi kutoka LANDESA akiwasilisha mapendekezo
yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya mipango ya
matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Kilimo
Afisa
Sheria kutoka NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo wakati
makundi mbalimbali wakiwasilisha maoni yao juu ya kanzi data
Afisa programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Kiombola akiwasilisha
mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya
mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Asasi za Kiraia.
Afisa wanyama pori (TAWA) Bw. Herman Nyanda akiwasilisha
mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya
mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Maliasili
Afisa Mpelembaji kutoka TNRF Bw. Wilbard akiwasilisha
mapendekezo yao kwa ajili ya mchakato wa uanzishwaji wa kanzi data ya
mipango ya matumizi ya ardhi kutoka katika kundi la Utafiti
Wadau wakiendelea na mkutano hu
No comments:
Post a Comment