Social Icons

Wednesday 3 January 2018

MELI YA WATALII 570 YATIA NANGA BANDARI YA DAR ES SALAAM.


Baadhi ya Watalii wakishuka kutoka kwenye meli ya kitalii ya kampuni ya Nautica Majuro katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii wakipiga picha “Selfie” punde baada ya kuwalisili katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii akicheza ngoma baada kunogewa na mrindimo wa ngoma ya utamaduni wa Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania imeshiki kutoa taarifa za utalii wa Tanzania kwa watalii takribani 570 waliowasili kwa meli ya kitalii ya kampuni ya Nautical Majuro katika Bandari ya Dar es Salaam .

Ujio wa Meli hii ya kitalii ni mwendelezo wa juhudi zinazofanywa kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania kwa dhamira ya kuwajulisha watalii kutoka katika nchi mbalimbali duniani kuwa wanaweza kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania kwa kutumia njia mbali mbali za usafiri (meli, ndege na njia ya barabara).

Watalii hawa wameweza kutembelea Pori la Akiba la Selous, eneo la Mlima Kilimanjaro, Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo na jiji la Dar es Salaam.

Meli hii imeanza safari zake katika bara la ulaya imewasili Tanzania tarehe 2/01/2018 saa 2 asubuhi na kuondoka saa moja usiku.

No comments: