Social Icons

Monday, 22 January 2018

MTANDAO WA ELIMIKA WIKIENDI WA KWENYE TWITTER SASA WALETA TOVUTI YA JUKWAA LA MAJADILIANO

Ili Kujiunga na Mtandao huu wa Elimika Wikiendi Bofya hapa www.elimika.co.tz 
Kwa ufupi
#ElimikaWikiendi ilianzishwa mnamo tarehe 15.01.2016 kama jamvi wazi kwa wapenda Kiswahili ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu jamii zao
 Kutafiti,kuhoji,kufahamiana,kujifunza mambo kadha wa kadha ikiwemo ubunifu wa Tehama, elimu juu ya afya, maendeleo jamii,ujasiliamali, mitindo, michezo na mengine mengi.

#ElimikaWikiendi hufanyika kila jumamosi kwa njia ya Twitter kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana kupitia #tag #ElimikaWikiendi . Saa moja la kwanza huwa ni wakati wa kukienzi Kiswahili kwa misemo,nahau,mafumbo na methali tofauti, na ikifuatiwa saa nyingine kwa ajili ya elimu juu ya afya kutoka kwa wataalam mbalimbali, Ikimalizia na masomo mchanganyiko ikiwa ni pamoja na teknolojia,maendeleo ya jamii au mada tofauti zenye mlengo wa kuelimisha jamii. 
Muonekano wa Tovuti ya Elimika Wikiendi



Baadhi ya Jumbe mbalimbali ambazo zilitumwa wakati wa kutambulisha rasmi Tovuti ya Elimika Wikiendi.
Ili Kujiunga na Mtandao huu wa Elimika Wikiendi Bofya hapa www.elimika.co.tz 
 Twitter @EW_Tanzania

No comments: