Mratibu
mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akiongea na
vijana Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masul waliochaguliwa
kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii
(ECOSOC) jijini New York kabla ya kuwakabidhi bendera ya Tanzania na
Umoja wa Mataifa.
Baraza
hilo linakutanisha vijana viongozi kutoka ulimwenguni kwote kujiunga na
waunda sera kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika
nchi wanazotoka na jinsi ya kuzitatua. Pia Mkutano huo unatoa fursa kwa
vijana kutoka nchi balimbali kubadilishana ujuzi wa namna ya kutatua
changamoto za vijana katika nchi zao. Mkutano
huo utafanyika kuanzia Jumatatu ya Januari 30 hadi 31 na unaweza kupata
tarifa za safari ya Rahman na Paschal kwa kufuatilia akaunti za Umoja
wa Mataifa katika Twitter @UnitedNationsTZ na Instagram @unitednationstz Bw.
Rodrguez akiwakabidhi vijana mfano wa hundi kama mchango wa Umoja wa
Mataifa Tanzania ili kuwawezesha vijana hao kuhudhiria Baraza la Uchumi
na Jamii (ECOSOC). Bw.
Rodrigues akiwakabidhi Rahma na Paschal bendera za Tanzania na Umoja wa
Mataifa kama utambulisho wao kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC). Mratibu
mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha na Rahma
pamoja na Paschal wakiwa wameshika bendera ya Umoja wa Mataifa Tayari
kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii
(ECOSOC).
Umoja
wa Mataifa Tanzania wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania kwenye
Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New York Rahma
Mwita Abdallah na Paschal Masulu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa
Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York.
Wawili
hao walichaguliwa kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa
kupitia mitandao ya kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya dakika
moja wakieleza kwanini wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa Tanzania
kwenye Baraza la ECOSOC.
No comments:
Post a Comment