Social Icons

Monday, 28 May 2012

TWIGA STARS YACHAPWA UGENINI 2-1 NA ETHIOPIA






TIMU ya taifa ya
wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza ‘vibaya kidogo’ kampeni za
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa wanawake,
baada ya kufungwa mabao 2-1 jana jioni mjini Addis Ababa na wenyeji,
Ethiopia.
Twiga sasa
inahitaji ushindi wa 1-0, Juni 16, katika mchezo wa marudiano mjini Dar
es Salaam, ili kukata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa mara ya pili
mfululizo, Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane
katika historia ya michuano hiyo

No comments: